Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi
Akinamama wengi
wa Tarafa ya Mwese katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda katika Mkoa wa Katavi wanalazimika
kujifungulia nyumbani kufutia kunyimwa
huduma kwenye kiliniki baada ya kushindwa
kwenda na waume zao kupimwa afya
zao
Hayo yalielezwa hapo jana na Diwani
wa viti maalumu wa Tarafa
hiyo Thiodela Kisesa kwenye kikao
cha Baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo kilichofanyika kwenye ukumbi
wa idara ya maji
Diwani Kisesa
alisema akinamama wajawazito wa Tarafa
hiyo wamekuwa wakikosa huduma ya kupimwa
maendeleo ya afya zao pindi waendepo
kupima afya zao kwenye kiriniki baada ya watowaji hoduma
kuwakatalia kuwapatia huduma za vipimo mpaka wawe wamekwenda na waume zao
Alisema wanaume wengi
wamekuwa wakitakiwa kwenda na
wake zao kupima afya zao na wake zao ilikuza kubaini napema
kama mama mjamzito anamaambukizi ya VVU ili kuokoa vifo vya mama na mtoto
Alifafanua baada
ya kuwa ya kukosa huduma hiyo ya
kiliniki akinamama wengi wamekuwa wakilazimika
kujifungulia majumbani kwao hari ambayo inafanya uhai wa mama na mtoto
kuwa mashakani
Kwa upande wake
mganga mkuu wa Wilaya ya Mpanda Joseph Msemwa
alilieleza baraza la madiwani kuwa jukumu la kupimwa afya sio la mama
peke yake bali ni la mama na baba
Alisema wapo
wanaume wanajua kwamba mama akipimwa na akinekana hana maambukizi ya VVU ajua
kuwa na yeye pia hana maambukizi jambo ambalo sio sahihi hata kidogo
Alifafanu kuwa akinama wote ambao ni wajawazito hata
kama hawakwenda na waume zao kiriki wanayo haki ya kupatiwa huduma ya vipimo
kama kaida bila kujali hata kama akwenda na mume wake

No comments:
Post a Comment