Friday, June 20, 2014

HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA KUWAPATIA WAZEE 710 VITAMBULISHO VYA AFYA YA WAZEE‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

N a  Walter  Mguluchuma
Mpanda Katavi
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi  imekamilisha  vitambulisho  710 kwa ajili ya  kuwapatia wazee kwa ajiri ya vitambulisho  vya  huduma  ya Afya kwa wazee
Hayo  yalielezwa hapo jana na Mganga  Mkuu wa Wilaya  ya Mpanda  Dr Joseph  Mkemwa  wakati wa kikao cha Baraza  la madiwani  wa Halmashauri ya Wilaya  ya Mpanda kilichofanyika  kwenye ukumbi wa Idara ya maji mjini  hapa kilichoongozwa na mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Yassin Kibeliti
Alisema  zoezi hilo la kuwapatia wazee vitambulisho  vya afya litakuwa ni endelevu  kwa ajiri ya kuwawezesha wazee waweze  kupata matibabu  bure kwenye Hospital   vituo vya Afya na kwenye Zahanati
Alifafanua  kwa kutambua umuhimu wa wakuwapatia  huduma ya  ya  matibabu bure wazee msimu ujao wa mwaka  wa fedha  wa 2014 na 4015  zimetengwa jumla ya shilingi milioni  saba kwa ajiri ya  shughuli za  kutengeneza vitambulisho vingine  vya huduma ya  afya ya wazee
Alisema  mwaka ujao wa fedha wanatarajia  kufika  kwenye maeneo mengi zaidi kwa lengo la  kuwaandisha wazee ili waweze kunufaika na utaratibu wa wa kupatatiwa matibabu bure
Kwa upande wake Diwani wa Viti maalumu  Thiodola Kisesa  alishauri kuwa ni vema vitambulisho hivyo vikaongezwa kwani idadi ya wazee huongezeka   mwaka hadi  mwaka
Nae Diwani wa Kata ya Mpanda Ndogo Hamad Mapengo  aliomba  zoezi la  usambazaji wa vitambulisho  vinapokuwa vimekamilika  viwe vinasambazwa kwa wakati   na kwenye  vijiji  vyote husika
Alisema  kumekuwepo na malalamiko kwa baadhi ya wazee kulalamikia  kucheleweshewa kupatiwa vitambulisho vyao pindi vinapo kuwa vimekamilika
Mkurugenzi  wa Halmashauri   Estomihn Chang’ah alisema  tatizo la ucheleweshaji wa upatikanaji kwa wakati  vitambulisho hivyo  husabishwa na muandaaji ambae amekuwa avitowi kwa wakati hata hivyo  tatizo hilo litamalizika hivi karibuni

No comments:

Post a Comment