Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mwanamke mmoja
aliyefahamika kwa jina la Mwashi
Ngehu(38) Mkazi wa Kijiji cha Chamalendi
Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya
Mlele Mkoa wa Katavi amefariki
Dunia kwa kujinyonga
kwa kutumia khanga baada ya kupatwa na hasira ya kufiwa na mtpto
wake wa Kike
Kwa mujibu wa
Kamanda wa jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari tukio hilo lilitokea hapo jana majira ya saa
kumi na moja alifajiri Kijijni hapo
Katika tukio hilo
ni kwamba marehemu marehemu alikuwa akimuuguza mwanae wa kike kwa muda wa
miezi miwili ambae alikuwa ni mtoto pekee wa marehe huyo
Alisema ndipo
hapo juzi mwae huyo alifariki dunia na
kuzikwa kijijini hapo na muda wote wa msiba
marehemu alikuwa akilia kwa uchungu
kufiwa na mwanae huyo wa pekee
Kidavashari
alieleza marehemu alikuwa akiwaeleza waombolezaji waliofika
kufariji msibani kuwa amepatwa na uchungu sana kufiwa na mtoto
wake ambae alimzaa kwa shida
sana kwani waliishi na mume wake
kwa muda mrefu bila kujaliwa kupata mtoto
Alisema marehemu
alikuwa akiwaeleza waombolezaji kuwa haoni faida ya kuishi tena Dunia bila kuwa na mtoto yoyote yule
Alieleza ndipo
hapo juzi majira ya usiku wakati alipokuwa
amelala ndani ya nyumba yake alipotoka
nje na kuwaaga ndugu zake waliokuwapo
msibani hapo kuwa anatoka nje kwenda kujisaidia
Alisema
marehemu hakurejea tena ndani ya nyumba
hadi hapo juzi majira ya saa kumi na moja mwili wake ulipokutwa ukiwa unang’inia juu ya mti huku akiwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia khanga yake
Mwili wa marehemu
umeisha fanyiwa uchunguzi wa Kidakitari na wamekabidhiwa ndugu zake kwa ajiri
ya mazishi ambayo yalifanyika hapo jana
kijini hapo

No comments:
Post a Comment