Wednesday, June 18, 2014

HALMASHAURI HAMASISHENI WATU WAJIUNGE NA MFUKO WA BIMA YA AFYA NHIF‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na Walter Mguluchuma
Viongozi wa Halmashauri  za Mkoa wa Katavi  wametakiwa kuwahamasisha wananchi  wao kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF ) ili wananchi wao waweze  kupata matibabu kwa bei nafuu 
Wito huo umetolewa hapo leo  na Mkuu wa Mkoa wa Katavi  kwenye  maadhimisho ya siku ya  wadau  wa NHIF na CHFyaliofanyika  kwenye ukumbi wa Katavi Resort katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Mwandisi  Emanuel Kalobelo
Alisema umefika  wakati sasa wa kila Halmashauri  kuhakikisha inatunga sheria   ya kumtaka kila mwananchi ajiunge na mfuko wa Bima ya Afya (NHIF)
Alifafanua  wananchi wa Mkoa wa Katavi ambao idadi yao inafikia jumla ya watu 564000  wanaonufaika na mfuko huo ni watu 66,000 tuu ambao ndio wamejiunga na mfuko wa NHIF ambao ni sawa na asilimia 12 ya wakazi wote wa Mkoa wa Katavi
Hivyo ni muhimu  kwa kila Halmashauri  kuhakikisha  zinawahamasisha wananchi wao wajiunge na mfuko wa Bima ya afya ili waweze kupatiwa matibabukwa gharama ndogo    pindi wanapokuwa wameugua
Alisema Halmashauri ziweke  ajenda ya kudumu  kwenye ratiba yao ya vikao vyao  na kuhakikisha kila kikao wanazungumzia na kujadili namna ya kuhamasisha mfuko huo wa Bima ya Afya kwenye maeneo yao
Alieleza  Mfuko huo uweke  utaratibu wa kuwaweka  watu wenye sifa zinazositahili watumishi ambao  wanakuwa na sifa zinazositahili kwenye vituo vyao vyote vya kutolea huduma
Alisema wapo  baadhi ya watumishi ambao wamekuwa na tabia ya kuwanyanyasa  watu ambao wanatibiwa kwa kutumia kadi ya Bima ya Afya hivyo wanachama wanaofanyiwa hivyo ni vizuri wawe wanatowa taarifa mapema ili  watumishi hao waweze kuchukuliwa hatua za kinidhamu
Aidha alikemea tabia ya baadhi ya wanachama ya kuazimisha kadi zao kwa watu wengine ambao sio wanachama wa mfuko  hivyo tambia hiyo sio nzuri   na iashwe mara moja
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa  Hamis Mdee  alieleza  kuwa  lengo la kikao hicho cha siku ya wadau nikukutana  na wadau  na kujadiliana  na kupeana  taatifa   za utekelezajiwa shughuli  za mfuko wa  Bima ya Afya  kwa  kipindi cha   mwaka mzimana kutowa nafasi kwa wanachama kutowa maoni na ushauri  
Alisema mfuko huo mbali ya kutowa matibabu kwa wanachama wake pia inatowa mikopo kwa wanachama wake na taasisi mbalimbli  na hivi karibuni walitowa mkopo kwa Hospitali ya Wilaya ya Mpanda wa fedha za kununulia mashine ya Axrey
Mdee alieleza kuwa lipochangamoto la upungufu wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma  ambapo tatizo hilo linaweza kupungua kwa kiasi kikubwa endapo  kutakuwa na usimamizi  mzuri kwenye vituo vya  kutolea huduma
Alifafanua  lengo la mfuko wa Bima ya Afya ni  kuwa  na wanachama asimilia  30 ya watanzania wote ifikapo mwakani 2015 kwani kwa sasa wanawachama asilimia 15
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima aalisema atahakikisha  ifikiapo hapo mwakani asilimia 100 ya wakazi wa wilaya ya Mpanda watakuwa wamejiunga na kuwa wanachama  wa Mfuko wa Bima ya Afya

No comments:

Post a Comment