Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi
Kaimu Mkuu wa
Mkoa wa Katavi Paza Mwamlima ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda ameziagiza
Halmashauri zote zilizopo katika Mkoa wa
Katavi zihakikishe sekita zao
zinajikita kuelimisha jamii kwa
vitendo ili ili kuondoa umasikini kwa wakazi wa Mkoa wa Katavi
Kaimu Mkuu wa
Mkoa wa Katavi alitowa agizo hilo hapo jana wakati akifungua washa ya siku ya
Polisi iliyofanyika hapo juzi kwenye
ukumbi wa Super City uliopo mjini hapa
Mwamlimu alisema
Mkoa wa Katavi umebahatika kuwa na furusa nyingi lakini mpaka sasa hazijatumika ipasavyo kutokana na
wananchi kutoelewa umuhimu wa
kuzitumia furusa hizo
Alisema wakati
sasa umefika wa kila Halmashauri
kutafusili furusa zilizopo katika
Mkoa wa Katavi ili ziweze kuwanufaisha wananchi kiuchumi na kuwaondolea umasikini hivyo
wataalamu wakikite kwa wananchi
na kuwapatia elimu
Alifafanua kuwa Wakurugenzi wahakikishe wanashirikiana na wafanya biashara katika
kutafuta masoko ya mazao ya ndani
ya nchi na nje ya nchi kwani mazao mengi yamelundikana kwenye maghala kutokana na kutokuwa na kutokuwa na mbinu za wafanya biashara ya kutafuta masoko ya kuuzia
Alisema hari ya watu inapokuwa mbaya kiuchumi husababisha
kuwepo kwa uhalifu hivyo
ilikukabiliana na uhalifu ni vizuri
kuhakikisha hari ya uchumi kwa wananchi inakuwa nzuri
Alifafanua ilinchi yetu iendelee kuwa na amani
na usalama ni vema kukumbushana
na kutathimini nini
kinahitajika katika kuimalisha
ulinzi na usalama hapa nchini
kwetu
Alisema jeshi la
pilisi litafanikiwa kuondoa uhalifu endapo wataacha kufanya kazi kwa mazoea hivyo wanao wajibu kubadilika
fikira na kuleta tija
Kwa upande wake
mkuu wa Kitengo cha polisi jamii hapa nchini Kamishina wa Polisi Mussa Ally
Mussa alisema ni vema watu wakatambue
kuwa kazi ya polisi jamii sio kazi ya polisi peke yao hivyo wananchi wanao wajibu wakushirikiana na
jeshi la polisi kwenye jukumu zima la
polisi jamii
Alisema dhamila
ya polisi jamii sio hasa kupambana na
wahalifu bali dhamila kuu ya
polisi jamii ni kuzuia uhalifu usitokea
Alieleza jeshi la
polisi linakabiliwa na shangamoto mbalimbali
kama vile uchache wa Askari
pamoja na vitendea kazi mbalimbali
changamoto hii ambayo inayakabili
majeshi yote ya polisi ya nchi zote
duniani
Changamoto nyingine aliitaja kuwa ni utovu wa nidhamu kwa baadhi ya askari ambapo wapo
wengi wamekuwa wakipokea rushwa kwa kisingizio cha mshahara mdogo wakati sio kweli kwani serikali imejitahidi kuboresha mishahara ya askari kwa kuwapatia posho kila
mwezi
Kamishina Mussa
alieleza wapo baadhi ya Askari wamekuwa na tabia ya kuvuta sigara
barabarani huku wakiwa wamevaa sare
za jeshi la Polisi wakati ni kinyume
cha utaratibu askari wanaofanya hivyo ni wahuni
Nae mmoja wa
washiriki wa washa hiyo Thomas Ngozi alisema kuwa askari wa jeshi hilo
wanaoajiliwa siku hizi wamekuwa hawana maadili kutokana na askari wanao ajiliwa kuwa na umri mdogo
hivyo ni vema umri wa kuajiri ukaongezwa
kutoka miaka 18 hadi miaka 20
No comments:
Post a Comment