Monday, June 16, 2014

VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUWAHAMASISHA WAUMINI WAO KUACHA UHALIFU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Mpanda Katavi
Viongozi wa madhehebu   yote ya Dini zilizopo hapa Nchini  wameombwa  kuwahamasisha waumini wao  waache  kufanya  vitendo  vya uharifu
Wito huu umetolewa hapo juzi  na mkuu wa kitengo cha Polisi  jamii wa Jeshi la Polisi  kamishina Mussa  Ally Mussa  wakati wa washa ya siku moja ya siku ya Polisi  iliofanyika kwenye ukumbi wa Super city  ulioko mjini Mpanda
Alisema  viongozi wa madhehebu ya Dini wanayonafasi kubwa ya kupunguza uhalifu hapa nchini  endapo  watawahamasisha  waumini wao  kwenye  madhehebu yao waache kufanya vitendo vya uhalifu
Kamishina Mussa   alieleza  wapo watu wanaofanya vitendo vya uhalifu kwasababu hawaubiliwi neno la mungu  ndio maana hawaogopi  kufanya uhalifu kwa kuwa hawamjuwi mungu
Aidha aliwataka  Askari polisi kuacha tabia ya kuwatolea watu lugha  mbaya pindi wanapo kuwa  wamekwenda kwenye vituo  vyao vya polisi  kwa lengo la kupatiwa huduma
Alisema  wapo baadhi ya Askari polisi  wamekuwa  na  tabia ya kuwatolea lugha  mbaya watu wanapokuwa wanahitaji kuhudumiwa  hali hiyo  inafanya kupunguza ushilikiano baina ya wananchi na jeshi la polisi
Aliwaomba  wananchi  wasiwe na tabia ya kuwaonea huruma  polisi  pale ambapo wanapo waona wanapokea Rushwa  hivyo ni vizuri wakatowa ushilikiano kwa kutowa taarifa  ili Rushwa ikomeshwe  ndani ya jeshi la polisi
Kwa upande wake mmoja wa  wshiriki wa washa hiyo  muhifadhi wa hifadhi ya mbuga ya Taifa ya Katavi Denis Mushi  alishauri   viongozi wa madhehebu ya Dini  kwenda kwenye maeneo ambayowanaishi watu   siyo rasimu kwenye mapori  na kuwahubilia  watu  waache uhalifu
Nae meneja wa mfuko wa hifadhi ya wa watumishi umma(PSPF) wa Mkoa wa Katavi Elneti Mawalla  ambae pia  ni wakiri  wa kujitegemea  Mkoani hapa alisema watuhumiwa  wengi wanaopatikana na tuhuma za kesi za mahuma za  kesi za mauwaji niwale ambao hawana dini hata majina yao yamekuwana ni yaajabuajabu  tuu kotokana na kutokuwa na dini
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda Selemani Lukanga aliwaeleza washiriki wa washa hiyo kuwa Halmashauri yake imepanga kuajiri askari  wake hivi karibuni watakaokuwa wanashirikiana polisi  kufanya kazi ya kuzuia uhalifu na kumbambana na uhalifu katika maeneo ya mji wa Mpanda

No comments:

Post a Comment