Home » » Auwawa kwa kushambuliwa na shoka wakati akila chakula na familia yake‏

Auwawa kwa kushambuliwa na shoka wakati akila chakula na familia yake‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 




Na  Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
 Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la  Charles  Mkimbili (60) wa Kijiji cha Kaulolo   Tarafa ya Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi  ameuwa  kwa kukatwa  na shoka kichwani  na mtu asiyefahamika  wakati  wakati akila  chakula cha jioni  na familia yake
 Tukio hilo la mauwaji ya kinyama lilitokea hapo juzi   majira ya saa mbili usiku kijini  hapo  nyumbani kwa marehemu  Charles  Mkimbili
Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi  wa Mkoa wa Katavi Kamishina Msaidizi Mwandamizi Dhahiri Kidavashari  alisema tukio hilo  lilitokea  nyumbani  kwake na marehemu  wakati akiwa anakula chakula  cha  jioni  akiwa na familia yake
Alisema  wakati marehemu akiwa  anakula chakula na familia yake  ghafla  alitokea mtu mmoja  mwanaume  akiwa  amejifisha sura yake huku akiwa ameshika shoka mkononi
Kamanda Kidavashari  alieleza  mtu  huyo  baada ya kuwa  kufika hapo  walipokuwa wakila chakula  alianza kumshambulia marehemu kwa kumkata  na shoka  kichwani  sehemu ya kisogo  na usoni  huku  familia yake ikiwa inapiga matowe ya kuomba msaada kwa majirani
Alisema  mtu huyo baada ya kuona mayowe yanazidi aliamua kukimbia na  kutokomea  mahari kusiko julikana huku akiwa amebeba shoka lale
Alifafanua  majirani walifika kwenye eneo hilo na  kumkuta marehemu akiwa  amegalagala chini huku akiwa tayari ameisha fariki Dunia na pembeni yake damu zikiwa zimetapakaa
 Kamanda Kidavashari  alisema  chanzo cha mauwaji hayo  bado hakijajulikana  hivyo Jeshi la Polisi linaendelea  na upelelezi  wa tukio hilo  na kuhakikisha  linawatia  mbaroni wahusika  wa tukio  hili  ili waweze  kufikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa