Home » » Auwawa kwa kukatwa na mapanga akiwa amelala ndani ya nyumba yake‏

Auwawa kwa kukatwa na mapanga akiwa amelala ndani ya nyumba yake‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mtu mmoja  aliyefahamika kwa jina  la  Mwaniroma  Nzura (53) Mkazi wa Kijiji  cha Kawanzige Kata ya Kakese Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi umeuwawa kwa kukatwa na mapanga wakati akiwa ndani ya nyumba yake akiwa amelala  na watoto wa mdogo wake
Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina Msaidizi Mwandamizi Dhahiri Kidavashari tukio hilo lilitokea  tarehe  moja june mwaka huu  majira ya saa  saba usiku nyumbani kwa marehemu kijijini   hapo
Alisema siku hiyo ya tukio marehemu  alikuwa amelala nyumbani kwake  na watoto wawil wa mdogo wake   waitwao  Mwajuma  Shururu (4) na  Amosi Shururu(3
Alieleza ndipo wahuaji hao  wasio fahamika  walipovunja mlango  wa nyumba hiyo ya marehemu na mlango huu uliangukia ndani ya nyumba    ambapo  iliwafanya waweze kuingia ndani ya nyumba huku marehemu akiwa amelala usingizi
Kamanda Kidavashari  alisema  baada ya wauaji hao  wasiofahamika kuingia ndani walianza kumshambulia  marehemu  Mwiniromwa kwa mapanga  sehemu za kichwani  huku watoto wa mdogo wake wakiwa wanashudia kitendo hicho
Baada ya  ya kumshambulia kwa kumkatakata na mapanga  wahuaji hao walipohakisha kuwa Mwiniromwa  ameisha  fariki dunia  walitokomea  gizinahuku watoto hao  wakiwawaendelea kupiga mayowe ya kuomba msaada kwa  majirani ambao walifika kwenye eneo hilo  na kumkuta marehemu akiwa ameisha fariki Dunia
Kamanda Kidavashari  amesema  watuhumiwa wa tukio la mauwaja  hayo bado hawaja kamatwa na jeshi la polisi linaendelea na msako wa kuwabaini wauwaji wa mauwaji hayo ya kinyama
Aidha jeshi la polisi mkoa wa Katavi  limetowa wito kwa wananchi  kuendelea kushirikiana na jeshi  la polisi  katika kuimarisha  ulinzi na usalama  katika Mkoa wa Katavi ikiwa  na pamoja  na kupinga  vitendo vya  mauwaji ya kikatili  kwa kutowa taarifa kwa jeshi la polisi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa