Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Katavi watapatiwa mafunzo yauandishi wa habari za kuhusu usimamizi wa sheria ya chakula ,dawa na vipodozi mafunzo ambayo yameandaliwa na (TFDA )
Mafunzo hayo ambayo yatawashirikisha waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari pamoja na wahariri yatamepangwa kufanyika kesho jijini Mbeya
Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA)imeandaa mafunzo hayo ya siku moja ambayo yatafanyika kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa ulioko jijini Mbeya
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Severe kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa TFDA mafunzo hayo pia yatawashirikisha waandishi wa habari na wahariri wa vyombo mbalimbali wa wa Kanda ya Nyanda za juu Kusini
Kusudi la mafunzo hayo ni kuwapatia waandishi wa habari uwezo wa uelewa juu ya mahitaji ya sheria ya chakula ,dawa na vipodozi sura ya 219
Mafunzo hayo yatawawezesha waandishi wa habari kutambua wajibu wa vyombo vya habari vinavyoweza kudhibiti matangazo ya bidhaa za chakula ,dawa na vipodozi na vifaa tiba ili kulinda afya ya jamii
Lengo jingine la mafunzo hayo ni kulinda afya za wananchi kwa kuzuia athari ambazo zinaweza kujitokeza kutokana na matumizi ya chakula ,vipodozi na vifaa tiba ambapo waandishi wa habari kwa kutumia taaluma yao wanayo nafasi kubwa ya kuielimisha jamii kulinda afy ya jamii
0 comments:
Post a Comment