Tuesday, May 20, 2014

WAANDISHI WA HABARI WA MKOA WA KATAVI KUPATA MAFUNZO YA TFDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Katavi  watapatiwa mafunzo yauandishi wa  habari  za kuhusu  usimamizi  wa sheria  ya  chakula  ,dawa na  vipodozi   mafunzo ambayo yameandaliwa na (TFDA )
Mafunzo hayo ambayo yatawashirikisha waandishi wa habari wa vyombo  mbalimbali vya habari  pamoja na wahariri  yatamepangwa  kufanyika  kesho jijini Mbeya
Mamlaka  ya chakula  na Dawa (TFDA)imeandaa   mafunzo hayo ya siku moja ambayo yatafanyika    kwenye Ukumbi wa  Benjamin Mkapa ulioko jijini Mbeya

Kwa  mujibu wa taarifa iliyotolewa na  Severe  kwa niaba  ya mkurugenzi mkuu  wa  TFDA  mafunzo hayo  pia yatawashirikisha waandishi wa habari na wahariri wa vyombo mbalimbali wa   wa Kanda ya Nyanda za juu Kusini
Kusudi la  mafunzo  hayo ni kuwapatia waandishi wa habari uwezo  wa uelewa  juu ya mahitaji  ya sheria  ya chakula ,dawa na vipodozi  sura ya 219
Mafunzo hayo  yatawawezesha  waandishi wa habari  kutambua  wajibu wa vyombo vya habari  vinavyoweza  kudhibiti  matangazo  ya bidhaa za chakula ,dawa na  vipodozi  na vifaa  tiba  ili  kulinda  afya ya  jamii
Lengo jingine la mafunzo  hayo ni  kulinda  afya za wananchi  kwa kuzuia  athari  ambazo zinaweza  kujitokeza  kutokana  na matumizi  ya chakula ,vipodozi  na vifaa tiba ambapo waandishi wa habari kwa kutumia taaluma yao wanayo nafasi kubwa ya kuielimisha jamii kulinda afy ya jamii

No comments:

Post a Comment