Tuesday, November 12, 2013

HII HATARI SANA: AKATWA SEHEMU ZA SIRI AKIWA AMELALA KWA SHEMEJI YAKE‏, SOMA KISA HIKI HAPA

N a Walter Mguluchuma-Katavi yetu Blog
Mpanda Katavi
Mtu mmoja Mkazi wa Kijii cha Majimoto Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi Mwami M wanalusi (31) amekatwa na kisu katika sehemu zake za siri na watu wasiojurikana wakati akiwa amelala ndani ya nyumba ya shemeji yake na watu wasio julikan.

Kamanda wa Polisi wa  Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema tukio hilo lilitokea hapo jana majira ya saa nane usiku nyumbani kwa shemeji yake.

Alisema siku ya tukio  Mwami  alikuwaameenda  kumtembelea  shemeji yake aitwaye  Anset  Kapampala (36) ambae alikuwa akiishi katika kijiji hicho cha Majimoto.

Baada ya mlo wa usiku mwenyeji wake alimuonyesha chumba cha kulala ambacho hata hivyo hakikuwa na godoro wala kitanda bali kulikuwa na Benchi la kupumzikia ambalo shemeji yake ambae ni mwenyeji wake alimweleza Benchi hilo ndilo alitumie kama kitanda cha kulalia kutokana na hari yake ya kiuchumi kutokuwa nzui.

Alisema wakati Mwami yuko ndani ghafla walitokea watu asio wafahamu ambao waliingia ndani ya chumba hicho  na wala hawakumsemesha chochote hari ambayo ilimfanya ashikwe na butwaa
Alieleza ndipo watu hao walipo anza kumkata kwa kisu sehemu zake za ume hadi ume ukawa umeharibika vibaya  na kisha watu hao wakatokomea kusiko julikana  na kumfaya yeye apige mayowe  ambapo shemeji yake  ambae alikuwa amelala kwenye nyumba yake nyingine  alishituka na ndipo alipoingia ndani na kumkuta mgeni wake akiwa ameharibiwa vibaya sehemu zake za siri
Kamanda Kamanda Kidavashari alisema chanzo cha tukio hilo  bado hakijulikana  na polisi wanaendelea na epelelezi ili kuwabaini  na kuwakamata waliohusika ili sheria  ichukuwe mkondo wake. 

Tukio Rasmi katika picha linakuja.,..

IKIWA KAMA KUNA GAZETI LINAHITAJI KUTUMIA HABARI HII TAFADHALI WASILIANA NASI KWA NAMBA HIZI 0654221465

No comments:

Post a Comment