Thursday, November 14, 2013

HOT NEWS: BUNDUKI YA SMG YASALIMISHWA NYUMBANI KWA AFISA MTENDAJI‏

N a Walter Mguluchuma-Katavi yetu Blog
Mpanda Katavi
Watu wasiofahamika wamesalimisha silaha Bunduki  aina ya Sub Machine  Gun  katika kijiji cha Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi ikiwa na magazini moja ambayo haikuwa na risasi nyumbani kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho cha Inyonga Abiud  Vilima
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema tukio hilo la kusalimisha silaha lilitokea hapo jana majira ya kumi na mbili asubuhi nyumbani kwaafisa mtendaji huyo
Alisema siku hiyo  watu wasiofahamika walisalimisha Bunduki hiyo usiku nyumbani kwa Abiud  wakati yeye na familia yake wakiwa wamelala usingizi ndani ya nyuma yao pasipo kujua
Kidavashari alieleza ndipo ilipotimia majira ya saa kumi na mbili Asubuhi majirani wa mwenyekiti huyo wa kijiji  wakati  wakiwa wanaelekea kwenye shughuli zao za maandalizi ya kilimo ndipo walipo iona Bunduki hiyo ikiwa imetelekezwa nyumbani kwa Afisa mtendaji wao wa Kijiji
Alisema ndipo walipomwamsha afisa huyo mtendaji ambae nae alishikwa na mshangao kuona silaha hiyo ikiwa imetelekezwa nyumbani kwake  hari ambayo ilimlazimu atowe taarifa kituo cha plisi cha Wilaya ya Mlele ambao walifika muda si mrefu na kuichukua silaha hiyo
Kidavashari alifafanua kuwa mafanikio hayo ya usalimishaji wa silaha huo umeyokana na elimu  ya polisi jamii inayoendelea kutolewa  na jeshi la polisi kwa wananchi katika maeneo mbalimbali hapa nchini
Pamoja na hofu ya wananchi juuya operesheni zinazoendelea hapa nchini kama vile Okoa maliasili na jeshi la polisi mkoa wa Katavi linaendelea na uchunguzi wa kuwabaini watu wanao miliki silaha kihalali na wanazitumia silaha zao kinyume na umilikaji wa vibari vyaoili waweze kuchukuliwa sheria dhidi yao 

KAMA KUNA GAZETI LINAHITAJI KUTUMIA HABARI HII WASILIANA NASI KWA NAMBA 0654221465

No comments:

Post a Comment