N a Walter
Mguluchuma-katavi yetu Blog
Mpanda Katavi
Watu wawili
wamekufa wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi katika matukio mawili tofauti ya ajali
ya pikipiki likiwemo la mwanafunzi mmoja kugongwa na pikipiki na kufa hapo hapo
wakati akitokea shuleni wakati akiendesha Baiskeli
Kwa mujibu wa
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari tukio la kwanza la
mwanafunzi wa shule ya msingi Mbungani Bundala
Shija (12) kugogongwa na pikipiki na kufa hapo hapo lilitokea hapo juzi majira ya saa kumi na mbili na nusu
asubuhi
Alisema siku hiyo
Bundala alikuwa ametoka nyumbani kwao akiwaanaelekea shuleni ya msingi Mbugani Kata ya Kakese alikuko kuwa
anasoma huku akiendesha baiskeli ndipoalipogongwa na pikipiki yenye namba
T937 CFF aina ya TOYO iliyokuwa ikiendeshwa na Kasansa
Protas (25) mkazi wa Kijijicha Kakese Mbugani Wilayani hapa
Alieleza mbali ya
mwanafunzi huyo kufa hapo hapo dreva wa Pikipiki nae aliumia vibaya kutokana na ajari hiyo na amelazwa katika
hospitali ya Wilaya ya Mpanda akiendelea kupatiwa matibabu huku akiwa chini ya
ulunzi wa Polisi
Katika tukio la pili
mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la
Geofrey Anatory Vicent 40
mkazi wa Mtaa wa Mpanda Hotel amefariki dunia baada ya kudondoka kwenye
pikipiki ambayo alikuwa amebebwa
Kamanda
Kidavashari alisema tukio hilo lilitokea hapo Novemba 10 mwaka huu katika eneo
la mtaa Nsemlwa kichangani mjini hapa
majira ya saa tano na nusu asubuhi
Alisema siku hiyo
ya tukio marehemu alikuwa amepanda pikipik yenye namba za usajiri T372 AXE iliyokuwa ikiendeshwa na
Armoury Seif Esry 32 mkazi wa
mtaa wa Madukani mjini hapa na baada ya kudondoka alifariki dunia hapo
hapo
Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi amewaonya waendesha vyombo vya moto wasio zingatia
sheria na taratibu za usalama Barabarani kuwa hatua kali za
kisheria zitachukuliwa dhidi yao
ili kunusuru watu wasiendelee
kuathilika na uzembe huo

No comments:
Post a Comment