Na Walter Mguluchuma
Mpanda
Katavi
Mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la Ngoro Nyengera
(60) mkazi wa Kijiji cha Mirumba Tarafa ya Usevya Wilaya ya Mlele Mkoa wa
Katavi ameuwawa kwa kukatwa kolomeo na
kitu chenye ncha kali nyumbani kwake
wakati akiwa amelala kitandani na mume wake.
Kwa mujibu wa
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema tukio hilo la
mauwaji ya mwanamke huyo ya kusikitisha lilitokea hapo juzi majira ya saa saba
na nusu usiku nyumbani kwa marehemu ambae alikuwa akiishi na mume wake aitwaye
Rina Kuzenza (70)
Alisema siku ya
tukio marehemu alikuwa amelala na mumewekitandani katika nyumba waliokuwa
wakiishi pamoja na kijana wao aitwaye
Ndura Kusenza (20) ambae yeye
alikuwa akilala chumba kinachotazamana na chumba cha wazazi wake.
Kamanda
Kidavashari alieleza ghafla watu wawili
walivunja mlango wa chumba alichokuwa amelala marehemu na mumewe na kuingia
ndani huku wakiwa na tochi kubwa mbili zenye mwanga mkali na kuwaweka chini ya
ulinzi wao marehemu na mumewe
Alisema ndipo
walipomwamuru mume wa Marehemu akifunike
usoni kwa shuka yake na kisha walimlazimisha alale akiwa amelala kifudifudi
Kidavashari
alieleza kuwa baada ya kulazimisha hivyo mumewe
alitekeleza amri hiyo na ndipo watu hao walipoanza kumkata Ngoro Nyengera
kolomeo hadi kufariki dunia
Kamanda Kidavashari
alisema siku za nyuma marehemu alikuwa akilalamikiwa na wanakijiji
wenzake kuwa ni mshilikina na
amekuwa akituhumiwa kuwaloga wanakijiji wenzake hari ambayo ilipelekea marehemu
kuchukiwa na kukosa mahusiano mazuri baina yake
na wanakijiji wenzake.
Alisema katika
tukio hilo hakuna mtu wala watu waliokamatwa na jeshi la polisi linaendelea
na upelelezi wa kuwabaini waliohusika katika mauwaji hayo ili kuweza
kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria kujibu tuhuma hii ya mauwaji ya kinyama
IKIWA GAZETI LOLOTE LINATAKA KUTUMIA HABARI HII WASILIANA NASI KWA NAMBA HIZI 0654221465
KATAVI YETU BLOG

No comments:
Post a Comment