N a Walter
Mguluchuma-Katavi yetu Blog
Mpanda Katavi
Mtu mmoja Mkazi
wa Kijii cha Majimoto Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi Mwami M wanalusi (31)
amekatwa na kisu katika sehemu zake za siri na watu wasiojurikana wakati akiwa
amelala ndani ya nyumba ya shemeji yake na watu wasio julikan.
Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari
alisema tukio hilo lilitokea hapo jana majira ya saa nane usiku nyumbani kwa
shemeji yake.
Alisema siku ya
tukio Mwami alikuwaameenda kumtembelea
shemeji yake aitwaye Anset Kapampala (36) ambae alikuwa akiishi katika
kijiji hicho cha Majimoto.
Baada ya mlo wa
usiku mwenyeji wake alimuonyesha chumba cha kulala ambacho hata hivyo hakikuwa
na godoro wala kitanda bali kulikuwa na Benchi la kupumzikia ambalo shemeji
yake ambae ni mwenyeji wake alimweleza Benchi hilo ndilo alitumie kama kitanda
cha kulalia kutokana na hari yake ya kiuchumi kutokuwa nzui.
Alisema wakati
Mwami yuko ndani ghafla walitokea watu asio wafahamu ambao waliingia ndani ya
chumba hicho na wala hawakumsemesha
chochote hari ambayo ilimfanya ashikwe na butwaa
Alieleza ndipo
watu hao walipo anza kumkata kwa kisu sehemu zake za ume hadi ume ukawa
umeharibika vibaya na kisha watu hao
wakatokomea kusiko julikana na kumfaya
yeye apige mayowe ambapo shemeji yake ambae alikuwa amelala kwenye nyumba yake
nyingine alishituka na ndipo alipoingia
ndani na kumkuta mgeni wake akiwa ameharibiwa vibaya sehemu zake za siri
Kamanda Kamanda
Kidavashari alisema chanzo cha tukio hilo
bado hakijulikana na polisi
wanaendelea na epelelezi ili kuwabaini
na kuwakamata waliohusika ili sheria
ichukuwe mkondo wake.
Tukio Rasmi katika picha linakuja.,..
IKIWA KAMA KUNA GAZETI LINAHITAJI KUTUMIA HABARI HII TAFADHALI WASILIANA NASI KWA NAMBA HIZI 0654221465

0 comments:
Post a Comment