Home » » AKAMATWA NA GOBOLE NA RISASI MBILI AKIMILIKI KINYUME CHA SHERIA‏

AKAMATWA NA GOBOLE NA RISASI MBILI AKIMILIKI KINYUME CHA SHERIA‏

Na Walter Mguluchuma-Blogzamikoa
Mpanda
Jeshi la polisi mkoa wa Katavi limemkamata Juma Nsokolo (32) mkazi wa kijiji cha Kashishi Tarafa ya Mpimbwe wilaya ya Mlele akiwa na silaha aina ya Gobole ikiwa na risasi mbili akimiliki kinyume cha sheria
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Katavi Emmanuel Nlay alisema mtuhumiwa alikamatwa hapo mei 23 mwaka huu majira ya saa 8 mchana
Alisema mtuhumiwa alikamatwa na silaha hiyo wakati akiwa katika harakati za kutaka kwenda kuwinda wanyama katika hifadhi ya taifa ya Katavi
Nlay alieleza baada ya mtuhumiwa kukamatwa na askari polisi na Askari wa hifadhi ya wanyama pori wa Katavi alikutwa pia na risasi mbili na fataki mbili
Mtuhumiwa alikamatwa na askari hao kufuatia dolia zinazoendelea katika mkoa wa katavi yenye lengo la kupambana na matukio mbalimbali yakiwemo ya ujangili.
Kaimu kamanda alisema uchunguzi wa tukio hili umekamilika na mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa