Na Walter Mguluchuma-Blogzamikoa
Mpanda
Jeshi la polisi mkoa wa Katavi limemkamata
Juma Nsokolo (32) mkazi wa kijiji cha Kashishi Tarafa ya Mpimbwe wilaya ya
Mlele akiwa na silaha aina ya Gobole ikiwa na risasi mbili akimiliki kinyume
cha sheria
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa
Katavi Emmanuel Nlay alisema mtuhumiwa alikamatwa hapo mei 23 mwaka huu majira
ya saa 8 mchana
Alisema mtuhumiwa alikamatwa na silaha hiyo
wakati akiwa katika harakati za kutaka kwenda kuwinda wanyama katika hifadhi ya
taifa ya Katavi
Nlay alieleza baada ya mtuhumiwa
kukamatwa na askari polisi na Askari wa hifadhi ya wanyama pori wa Katavi
alikutwa pia na risasi mbili na fataki mbili
Mtuhumiwa alikamatwa na askari hao
kufuatia dolia zinazoendelea katika mkoa wa katavi yenye lengo la kupambana na
matukio mbalimbali yakiwemo ya ujangili.
Kaimu kamanda alisema uchunguzi wa tukio
hili umekamilika na mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani
No comments:
Post a Comment