Walter Mguluchuma-Katavi yetu Blog
Jeshi la polisi mkoani katavi
limewakamata watu wawili katika matukio mawili tofauti wakiwa na pombe haramu
ya gongo lita 70
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa
Katavi Emmanuel Nlay aliwataja waliokamatwa kuwa ni Marietha Ngalawa (59) mkazi
wa kijiji cha Tukoma na January Katalambula (33) mkazi wa kijiji cha Mtisi wote
wanatoka wilaya ya Mlele
Katika tukio la kwanza Marietha
alikamatwa na lita 10 za pombe haramu ya gongo zikiwa zimehifadhiwa nyumbani
kwakwe
Kaimu kamanda Nlay alisema tukio hilo
limetokea hapo mei 21 mwaka huu majira ya saa 6 mchana.
Tukio la pili lilitokea hapo mei 25
majira ya saa 12 jioni ambapo January Katambala alikamatwa na lita 60za pombe
haramu ya gongo zikiwa zikiwa ndani ya nyumba yake.
Alieleza watuhumiwa hao walikamatwa
kufuatia taarifa zilizolifikia jeshi la polisi kuwa watu hao wanajishughulisha
na biashara haramu ya pombe aina ya gongo
Upelelezi wa matukio haya yote mawili
umekamilika na watuhumiwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamanai kujibu mashitaka
No comments:
Post a Comment