Home » » AKAMATWA GESTI NA MTAMBO WA KUTENGENEZEA NOTI BANDIA

AKAMATWA GESTI NA MTAMBO WA KUTENGENEZEA NOTI BANDIA

Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Jeshi la polisi mkoa wa  Katavi limemkamata   Hilali  Abdalah  (30)  mkazi wa  mtaa wa majengo  mjini hapa  kwa  kumkamata  akiwa na vifaa  vya kutengenezea noti  bandia   akiwa katika nyumba ya kulala wageni
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema Hilali alikamatwa hapo jana majira ya  ssa 8 mchana katika nyumba ya kulala wageni inaitwa  Ambassodor aliyoko  katika mtaa wa  mji wa  zamani  Kata ya kashaulili  mjini hapa
Alisema mtuhumiwa alikamatwa   kufuatia taarifa za kiitelejensia  kulifikia jeshi la polisi mkoa wa Katavi kutoka kwa raia wema  kuwa Hilali anajihusisha  na shughuli hiyo ya utengenezaji wa noto bandia
Kidavashari alivitaja vifaa aliwavyo kamatwa navyo   mtuhumiwa kuwa ni  karatasi ngumu  217 ambazo hutumika kutengenezea   noto bandia za  shilingi  10,000  bomba mbili  za sindano  zenye dawa maalumu  kwa ajiri ya kubadilishia  rangi  ya karatasi hizo  ili zifanane na pesa hizo
Alivitaja vifaa vingine kuwa ni  powder  chupa moja  kwa ajili ya  ya kumfanya mteja ataakizishika  mapema  zisiacche  alama ya vidole  kwenye pesa  beseni  moja jeusi  kwa ajiri ya kusafishia  karatasi hizo  mara baada ya kuzipitishia  kwenye hatua kadha
vifaa ningine alivyo kamatwa navyo  Hilali ni  karatasi 21  plain  kwa ajiri ya  kufunikia  karatasi ngumu  zisipate hewa  wakati wa utengenezwaji wa noti   bandia  soltap  2  kwa ajiri  ya kubania  karatasi  zisipate  hewa  mapema   pasi moja ya umeme  kwa ajili ya  kukaushia  pesa  hizo  mara  baada ya kuziosha na ugolo  vijiko vitatu   ambao alikuwa akiutumia kama kilevi  wakati akifanya shughuli hiyo  haramu
Kamanda waa polisi  mkoa wa  Katavi alieleza  awali  mtuhumiwa alikuwa akijishughulisha  na shughuli  za  kuuza  mitumba  kaika soko la Buzogwe  mjini hapa  na baadae  alihamia mkoani  Tanga  na ndiko aliko patia ujuzi wa kutengeneza noti bandia
Kidashari alieleza  hatimaye baada ya kupata utaalamu huo  alirejea Mpanda  na kuanza  kazi  hiyo  mbaya   ya   kuvunja sheria  za Nchi
Alisema katika  maelezo yake ya awalialikiri kufanya shughuli hiyo  kwa kile alicho kieleza ni kutokana   na yeye  hapo siku za nyuma aliwahi kutapeliwa  pesa kwa kupewa noto bandia ndio maana ameamua na yeye kulipa kisasi kwa watu wengine
Pia mtuhumiwa alitaja sababu nyingine kuwa ni katika kujitafutia maisha  kwa njia ya ytafuataji ndio maana akaamua   kujitafutia pesa kwa njia hii
mtuhumiwa anategemewa  kufikishwa mahakamani  mara upelelezi wa kesi hii utakapo kamilika ili aweze kujibu mashitaka yanayo mkabili

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa