Na Walter Mguluchuma
Mpanda
Katavi
Jeshi
la polisi mkoa wa Katavi limemkamata Hilali
Abdalah (30) mkazi wa mtaa wa majengo mjini hapa
kwa kumkamata akiwa na vifaa vya kutengenezea noti
bandia akiwa katika nyumba ya kulala wageni
Kamanda
wa polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema Hilali alikamatwa hapo
jana majira ya ssa 8 mchana katika nyumba ya kulala wageni inaitwa
Ambassodor aliyoko katika mtaa wa mji wa zamani Kata ya
kashaulili mjini hapa
Alisema
mtuhumiwa alikamatwa kufuatia taarifa za kiitelejensia
kulifikia jeshi la polisi mkoa wa Katavi kutoka kwa raia wema kuwa Hilali
anajihusisha na shughuli hiyo ya utengenezaji wa noto bandia
Kidavashari
alivitaja vifaa aliwavyo kamatwa navyo mtuhumiwa kuwa ni
karatasi ngumu 217 ambazo hutumika kutengenezea noto bandia
za shilingi 10,000 bomba mbili za sindano zenye
dawa maalumu kwa ajiri ya kubadilishia rangi ya karatasi
hizo ili zifanane na pesa hizo
Alivitaja
vifaa vingine kuwa ni powder chupa moja kwa ajili ya ya
kumfanya mteja ataakizishika mapema zisiacche alama ya
vidole kwenye pesa beseni moja jeusi kwa ajiri ya
kusafishia karatasi hizo mara baada ya kuzipitishia kwenye
hatua kadha
vifaa
ningine alivyo kamatwa navyo Hilali ni karatasi 21
plain kwa ajiri ya kufunikia karatasi ngumu zisipate
hewa wakati wa utengenezwaji wa noti bandia
soltap 2 kwa ajiri ya kubania karatasi
zisipate hewa mapema pasi moja ya umeme kwa ajili
ya kukaushia pesa hizo mara baada ya kuziosha na
ugolo vijiko vitatu ambao alikuwa akiutumia kama kilevi
wakati akifanya shughuli hiyo haramu
Kamanda
waa polisi mkoa wa Katavi alieleza awali mtuhumiwa
alikuwa akijishughulisha na shughuli za kuuza
mitumba kaika soko la Buzogwe mjini hapa na baadae
alihamia mkoani Tanga na ndiko aliko patia ujuzi wa kutengeneza
noti bandia
Kidashari
alieleza hatimaye baada ya kupata utaalamu huo alirejea
Mpanda na kuanza kazi hiyo mbaya
ya kuvunja sheria za Nchi
Alisema
katika maelezo yake ya awalialikiri kufanya shughuli hiyo kwa kile
alicho kieleza ni kutokana na yeye hapo siku za nyuma aliwahi
kutapeliwa pesa kwa kupewa noto bandia ndio maana ameamua na yeye kulipa
kisasi kwa watu wengine
Pia
mtuhumiwa alitaja sababu nyingine kuwa ni katika kujitafutia maisha kwa
njia ya ytafuataji ndio maana akaamua kujitafutia pesa kwa njia hii
mtuhumiwa
anategemewa kufikishwa mahakamani mara upelelezi wa kesi hii
utakapo kamilika ili aweze kujibu mashitaka yanayo mkabili
No comments:
Post a Comment