Home » » WANAWAKE MPANDA KUPEWA MAFUNZO YATAKAYO WASAIDIA KUWAPA UWEZO WA KUJITEGEMEA‏

WANAWAKE MPANDA KUPEWA MAFUNZO YATAKAYO WASAIDIA KUWAPA UWEZO WA KUJITEGEMEA‏


Na Walter Mguluchuma-Wa Blogs za Mikoa
mpanda
Akina mama wa wilaya ya mpanda mkoa wa Katavi wameandaliwa kupewa
mafunzo yatakayowapa uwezo wa kujitegemea kwenye maisha yao ya
kila siku
Hayo yalielezwa na mwenyekiti wa jumuia ya kina mama wa mkoa wa
Katavi Anna lupembe wakati alipo kuwaakiwahutubia akina mama wa
mji wa mpanda hapo jana kwenye ukumbi wa CCM Mpanda
Alisema vikundi vingi vya vikoba vilishindwa kuendelea kutokana
na kutotolewa kwa elimu kwanza ndio maana ameona awaletee
wataalumu watakao wapa uwezo wa kutambua umuhimu wa kujitegemea
Lengo la mafunzo hayo yaliyo andaliwa na yeye Lupembe ni kumfanya
kila mwanamke aweze kuwa na kipato chake yeye mwenyewe
Lupembe alisema mafunzo watakayo fundishwa ni utengenezaji wa
vitenge aina ya batiki chaki sabuni pamoja na ufugaji wa kuku
wa kisasa
Alieleza kuwa wataalamu hao ambao watashirikiana na wataalamu
kutoka Sido watakuwa wakitowa mafunzo kwa kupitia kwenye vikundi
kadri vitakavyo kuwa vimeandaliwa kwenye maeneo mbalimbali
Aidha aliwaeleza utaalamu ambao wakakao kuwa wameupata kewnye
mafunzo utawawezesha kuunda vikundi ambavyo vitawafanya waweze
kuwa na dhamamana kwenye taasisi za kibenki
Alisema taasisi za fedha zina shawishika zaidi kutowa mikopo kwa
vikundi kuliko kwa mtu mmoja mmoja na ni vizuri mkachagua
viongozi wa vikundi vyenu ambao ni waaminifu
Endapo mtakuwa na viongozi waaminifu mnaweza hata kushindwa
kurudisha fedha mnazo kuwa mmekopeshwa na tasisi za fedha
katika mkutano huo akina mama walitowa kero mbalimbali akiwemo ya
kuilamikia huduma mbovu zinazo tolewa kwenye wodi ya wazi ya
hospital ya wilaya ya Manda

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa