Home » » AKINAMAMA KATAVI WATAKIWA KUACHA TABIA YA KUCHUKIANA‏

AKINAMAMA KATAVI WATAKIWA KUACHA TABIA YA KUCHUKIANA‏


Na Walter Mguluchuma
Mpanda
Akinamama wa mkoa wa Katavi wametakiwa kuacha tabia ya kuchukiana
bila sababu kwani chuki ndio imekuwa chanzo cha mgawanyiko kwa
kinama wa mkoa wa Katavi
wito huu umetolewa hapo jana na Mwenyekiti wa akina mama wa CCM
wa Mkoa wa Katavi Anna Lupembe wakati alipo kuwa akiongea na
akina mama wa mji wa mpanda kwenye mkutano ulio fanyika jana
kwenye ukumbi wa CCM Mpanda
Alisema kitendo cha akina mama kuchukiana bila sababu kimekuwa
ndio chanzo cha akina mama wa mkoa wa katavi kushindwa kupata
maendeleo ya kweli
Lupembe ambae alikuwa ni mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Rukwa
aliye maliza muda wake alielaza kuwa endapo akina mama wa Mkoa wa
Katavi wataendelea kuwa na tabia ya kujengeana chuki upo
uwezekano mkubwa wa kugawanyika kwa akina mama
Alieleza kuwa ni vizuri akina mama wapendane na washirikiane
kwani chuki kamwe huwa hazileti maendeleo ya kweli kwenye jamii
ya watu
Pia aliwataka akina mama wawe na utaratibu wa kushiriki kwenye
mikutano ambayo inakuwa imeitishwa na viongozi wa serikali ili
muweze kujua yanayo kuwa yamejiri
Alifafanua kuwa mmekuwa mkikosa haki zenu za msingi kutokana na
kutohudhuria kwenu kwaenye mikutano ambako mgewaza kufikisha
kero zenu zinazo wakabili

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa