Na Walter Mguluchuma Mpanda
Waziri kuu wa Serikari ya jamhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Pinda ameondoo ukimya wa tuhuma zilizo tolewa dhidi ya makamu mwenyekiti wa Taifa wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Said Arfi zilizo tolewa kwenye mkutano wa mashauliano ya mikoa ya Katavi na Rukwa kuwa alimpa rushwa ili apite bila kupingwa kwenye jimbo lake wakati wa uchaguzi mkuu uliopita wa 2015.
Pinda aliondo ukimya huo hapo juzi wakati akiwahutubia wananchi wa mkoa wa Katavi wakati alipo kuwa akiwahutubia kwenye sherehe za kuuwaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013 zilizo fanyika kewnye ukumbi wa Idara ya maji wa halmashauri ya wilaya ya mpanda.
alisema ni vizuri (CHADEMA) wakaa wakamaliza migogoro iliyopo ndani ya chama chao kuliko kuendelea kuzushiana mambo ambayo hayana msingi wala ukweli ambayo yataendelea kukigawa chama hicho kama hawata kuwa makini.
Nimesikia kwenye mkutano wa mashauriano wa (CHADEMA) wa mikoa ya Rukwa na Katavi ulio fanyika wilayani Nkasi desemba 16 mwaka jana mwenyekiti wa (BAVICHA) wa mikoa hiyo alishutumu Arfi kuwa alihongwa hela na Pinda iliapite bila mpinzani.
Alisema yeye hakuhonga hera kwa Arfi na angehonga kwa nini wakati yeye katika maisha yake hajawahi kutowa rushwa wala kupokea na haipindi rushwa kabisa.
Alifafanua kuwa yeye na Arfi wamekuwa na ukaribu kutokana na shughuli zao za ubunge ambapo wamekuwa wakishirikiana katika kuwaletea maendeleo wa wananchi wa mpanda na mkoa wa Katavi kwa ujumla alisema Pinda.
Hotuba hiyo ya Pinda ameitowa kufuatia kuwa mkimya tangia huhuma zilizo tolewa na mwenyekiti wa (BAVICHA) wa mikoa hiyo Laulent Mangweshi alimpo mtaka Arfi akieleze kikao kicho alipokea rushwa ya shilingi ngapi kutoka kwa pinda wakati wa uchaguzi wa 2010
Hata hivyo kikao hicho cha mashauliano kilifikia uamuzi wa kumsimamisha uongozi mwenyekiti huyo wa (BAVICHA) na mara baada ya kikao hicho Arfi alikwenda (TAKUKURU) na kuiomba ifanye uchunguzi dhidi yake kuhusiana na tuhuma za kupokea rushwa kutoka kwa Pinda na akibainika ni kweli aliomba (TAKUKURU) imfikishe mahakamani.
No comments:
Post a Comment