Tuesday, January 15, 2013

BARAZA LA MADIWANI LA MJI WA MPANDA KUKUTANA ILI KUJADILI TUHUMA ZA UBATHILIFU WA FEDHA IKIWEMO YA SHANGINGI LA MKURUGENZI WA MJI LILILOGHALIMU MATENGENEZO YA TSHS MILIONI 40 NA MIRADI YA MAENDELEO.‏


Na Walter Mguluchuma.
Mpanda.

Baraza la madiwani la  Halmashauri ya mji  wa  mpanda  mkoa wa Katavi  limepitisha uamuzi  wa kuitisha   kikao  maalumu  cha daraza hilo  ili kujadili  tuhuma  zinazo ikaibili  Halmashauri hiyo  inayo  husuana na miradi mbambali   ikiwemo  ghama ya matengenezo ya  shangingi  la mkurugenzi  wa mji huo  lililo   fanyiwa matengenezo kwa ghama ya  shilingi milioni 40.

Uamuzi wa  kuitishwa kwa kikao   maalumu cha Baraza  la madiwani    ulipitishwa  na Baraza  hilo  katika kikao  chake kilicho  fanyika  desemda 31mwaka jana katika  ukumbi wa chuo kikuu huria cha mkoa wa Katavi.

Taarifa ya kufanyika kwa kikao  hicho ilitolewa hapo jana na mwenyekiti  wa Halmashauri ya mji wa mpanda Enock Gwambasa alipo kuwa  akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Alisema  katika kikao kilicho fanyika  desemba 31 mwaka jana  Baraza hilo  lilishindwa  kujadili taarifa ya kamati ya madiwami  iliyo  kuwa imepewa jukumu  la  kufuatilia huma za miradi  mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri yake  ambayo  ilikuwa na utata.

Uamuzi wa wakuitishwa kwa baraza maalumu  la madiwani  umezingatia   ukubwa wa  wa swala lenyewe  la  huhuma za  ubadilifu wa fedha  ambapo  taarifa ya kamati  ya madiwani  wameisha kamilisha taarifa hiyo yenye kurasa 22  ili madiwani waweze kuipitia kwa kina na kuijadili.

Alifafanua  kuwa kutokana na hari hiyo  Baraza la madiwani  waliamua  kupitisha  uamuzi  wa kuitishwa kwa  kikao maalumu  cha baraza la madiwani  ndani ya siku 14  baada ya kikao  hicho cha  desemba 31 mwaka jana.

Gwambasa alizitaja baadhi ya tuhuma za ubadilifu wa fedha    ni malipo ya  ya matengenezo  ya  gari  la mkurungenzi  wa Halmashauri hiyo  lenye namba STK5142 aina ya shangingi  lililo  ghalimu  matengenezo ya shilingi milioni 40  matengenezo yaliyo fanyika katika gereji  inayoitwa LWICHEya mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.


Katika malipo  ya matengenezo hayo yanayo  lalamikiwa kuwa ni makubwa  mkurugenzi wa  Halmashauri ya mji  wa mpanda Joseph Mchina  ana daiwa aliidhinisha  kulipwa kwa shilingi  milioni  25 za awali kwa mwenye gereji hiyo  kinyume  na utaratibu  wa mamlaka aliyo  nayo kama mkurungenzi  ambapo mamlaka aliyo nayo  yana mpa madaraka ya kuidhinisha malipo yanayo ishi  shilingi milioni 10 tuu.

Alieleza kuwa  malipo yoyote yanayo zidi   shilingi milioni 10  ni lazima yaidhinishwe  na kamati  ya fedha na mipango   utaratibu ambao    hakufuatwa katika malipo hayo.

Gwambasa alizitaja huma nyingine zinazo ikabili halmashauri ya mji  ni mradi wa ng’ombe wa wananchi wa kijiji cha Kakese ambapo  halmashauri  iliidhinisha  wanunuliwe ng’ombe wakubwa  lakini  inadaiwa  wamenunuliwa ndama kwa bei ya ng’ombe wakubwa  pamoja na mradi wa  ufugaji wa nguruwe katika  ya kawajense.

 Alitaja tuhuma nyingine kuwa  madai ya ujenzi  wa ghara la kuifadhia chakula katika kata ya Kakese linalo  daiwa kujengwa chini ya kiwango.

No comments:

Post a Comment