Thursday, January 17, 2013

WAZIRI MWANRI AWACHACHAMALIA WANAOPIGA MIMBA WANAFUNZI

IMG_6469
Na Kibada Kibada wa Fullshangwe-Katavi
Naibu  Waziri wa nchi  Ofisi ya waziri mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)  Agrey Mwanri amewaagiza viongozi na Watendaji wa serikali kuhakikisha wanakomesha suala la mimba mashuleni.
Waziri Mwanri alitoa agizo hilo (leo) wakati akizungumza na wananchi  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha  Kilida Kata ya Mamba wilayani Mlele Mkoani Katavi katika ziara yake ya kukagua na kuhimiza shughuli za maendeleo na kuona jinsi gani Halmashauri zinasimamia fedha za serikali zinazoletwa kwenye halmashauri kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika kutekeleza miradi na kupeana mikakati jinsi ya kusimamia fedha hizo ili zifznye kazi iliyokusudiwa.
 Amesema  ni wajibu wa viongozi kuhakikisha suala la mimba linakomeshwa kabisa mashuleni na haitoshi kila mara viongozi kuripoti tu, suala la mimba mashuleni bila hatua kuchukuliwa kwa wale wahusika wanaofanya vitendo hivyo vya kuwapa mimba watoto wa kike.
“Haitakiwi kuripoti tu,pia inatakiwa kueleza ni hatua gani zimechukuliwa  kuhakikisha hao wanofanya vitendo hivyo wamechukuliwa hatua zipi za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo”alisema kwa kufoka Mwaniri.
Aliagiza kufuatia kusomewa  taarifa ya Mkoa kuhusu maendeleo ya Mkoa  iliyosomwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Lauten Kanoni   ikieleza hali ya elimu na jinsi suala la mimba kwa watoto wa kike linavyo shughulikiwa
 Aidha katika taarifa hiyo ilieleza  hali ilivyo kwa sasa ilieleza kuwa mimba kwa mkoa wa katavi zimepungua kutoka wasichana waliopata ujauzito mwaka 2011  (63)  na  mwaka 2012  mimba zilipungua kufikia  (61)   sawa na asilimia tano .taarifa ambayo haikueleza namna wanavyolishughulikia tatizo la mimba na kueleza wangapi walichukuliwa hatua za kisheria kulingana na makosa hayo.
Na ni mikakati gani inafanywa kuhakikisha wanakomesha kabisa suala la mimba mashuleni kwa wanafunzi wengi wanapatiwa mimba na wazazi na jamii inaangali badala yake wanamalizana kwa kupeana zawadi huko huko majumbani hali hiyo inayofanya kuendelea kila mwaka.
 “Juhudi kubwa inatakiwa kufanyika ili kuhakikisha  wale wote wanaohusika wanachukuliwa hatua kali za kisheria kukomesha suala hili kwa kushirikiana wote viongozi wananchi, serikali, jamii, wazazi, walimu na wanafunzi kwa nafsi yao kukomesha suala la mimba kwa watoto wa kike mashuleni”alimaliza Mwanri.

No comments:

Post a Comment