Home » » PINDA AFUNGUKA KUHUSIANA NA TUHUMA ZA RUSHWA YA ARFI‏

PINDA AFUNGUKA KUHUSIANA NA TUHUMA ZA RUSHWA YA ARFI‏


Na Walter Mguluchuma Mpanda 

Waziri kuu wa Serikari ya jamhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Pinda ameondoo ukimya wa tuhuma  zilizo  tolewa  dhidi ya makamu mwenyekiti  wa Taifa wa chama cha Demokrasia  na Maendeleo  (CHADEMA) Said Arfi  zilizo tolewa kwenye mkutano wa mashauliano   ya mikoa ya Katavi na Rukwa kuwa alimpa rushwa ili apite bila kupingwa kwenye jimbo  lake wakati wa uchaguzi mkuu uliopita wa 2015.

Pinda aliondo ukimya huo   hapo juzi  wakati akiwahutubia wananchi  wa mkoa wa Katavi  wakati alipo kuwa akiwahutubia   kwenye sherehe za kuuwaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013 zilizo fanyika kewnye ukumbi wa Idara ya maji wa halmashauri  ya wilaya ya mpanda.

alisema  ni vizuri (CHADEMA) wakaa wakamaliza migogoro  iliyopo ndani  ya chama  chao  kuliko kuendelea  kuzushiana  mambo ambayo  hayana msingi  wala ukweli ambayo yataendelea kukigawa chama hicho  kama hawata kuwa makini.

Nimesikia  kwenye mkutano wa   mashauriano wa  (CHADEMA) wa mikoa ya  Rukwa na  Katavi  ulio fanyika wilayani  Nkasi  desemba 16 mwaka jana  mwenyekiti  wa (BAVICHA) wa mikoa hiyo alishutumu Arfi  kuwa alihongwa hela na Pinda iliapite bila mpinzani.

Alisema yeye  hakuhonga hera kwa Arfi  na angehonga  kwa nini  wakati yeye  katika maisha yake hajawahi kutowa rushwa  wala kupokea  na haipindi rushwa kabisa.

Alifafanua kuwa yeye  na Arfi  wamekuwa na  ukaribu  kutokana  na shughuli  zao za ubunge ambapo wamekuwa  wakishirikiana  katika kuwaletea  maendeleo wa wananchi wa mpanda na mkoa wa Katavi kwa ujumla  alisema Pinda.

Hotuba hiyo ya Pinda  ameitowa  kufuatia kuwa mkimya  tangia  huhuma  zilizo tolewa na mwenyekiti wa  (BAVICHA)  wa mikoa hiyo Laulent Mangweshi  alimpo mtaka Arfi akieleze kikao kicho  alipokea rushwa ya shilingi  ngapi kutoka kwa pinda wakati wa uchaguzi wa 2010

Hata hivyo kikao hicho  cha mashauliano  kilifikia uamuzi wa kumsimamisha uongozi  mwenyekiti huyo wa (BAVICHA)  na mara baada ya kikao  hicho Arfi  alikwenda (TAKUKURU) na kuiomba ifanye uchunguzi dhidi yake  kuhusiana na tuhuma  za kupokea rushwa kutoka kwa Pinda na akibainika  ni kweli  aliomba  (TAKUKURU) imfikishe mahakamani.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa