Tuesday, January 15, 2013

DC NKANSI AWAHIMIZA WAANDISHI WA HABARI KUANDIKA HABARI ZISIZOWEZA KUWAGAWA WANANCHI‏


Nawalter  Mguluchuma
Sumbawanga

Waandishi wa  wa mikoa ya katavi na Rukwa  wametakiwa kuepukana na  kuandika   habari  ambazo  ambazo  zina weza kusababisha   uvunjwaji wa amani  hapa nchini  hivyo ni  vizuri  wakatanguliza  uzalendo kwanza

Ushauri huu umetolewa hapo jana na Mkuu wa wilaya ya Nkasi Idd Kimanta alipo kuwa akifungua  mkutano mkuu wa chama cha waandishi wa habari wa mkoa Rukwa (RKPC) hapo jana katika ukumbi wa chama cha waalimu  mkoa wa Rukwa ulio washirikisha  pia waandishi wa habari kutoka mkoa wa Katavi

Alisema  waandishi wa habari ni watu ambao jamii inawaamini  sana  hivyo  wanapo  tumia vibaya taaluma hiyo   wanaweza wakasababisha  kuvunjika kwa amani  kutokana  na imani  walio nayo  juu yao

Alifafanua kuwa  wana hababari  ni vizuri  wakawa ni watu wakutenda mema  kwenye jamii  ya watu na watu watawapenda  na kujenga imani  kwa wanahabari
Kimanta aliwataka waachane  na kufanya kazi kwa mazoea  bali wafanye kazi kwa kufuata tija

Pia aliwaomba washirikiane na jamii inayo wazunguka  ili kuimalisha  mausano  hivyo wasiwe ni watu wanao jiona
Alisema  waandishi wa habari  waejiepushe na kutumiwa na watu  kwa kuwatumia vibaya kuchafua watu  na wengine kuwapa sifa ambazo  hawana  na wasipende kuandika habari za viongozi tuu bali waandike  na maswala ya Vijijini

jitahidini  kujielimisha  na elimu mbambali  ili muweze kubobea  kwenye taaluma hiyo  sio kila mwandishi  wa habari  sio  kila mwandishi anaweza kuandika vizuri  habari  mbazo haja zibobea  someni  uhumi  someni afya  elimu na michezo alisema  mkuu huyo wa wilaya ya Nkasi

Nae msoma risara Juddy Ngonyani  akisoma risala hiyo   kwa mgeni rasimi wa mkutano huo mkuu wa waandishi wa habari  alisema kuwa waandishi wa habari wa mikoa hiyo  ya Rukwa na Katavi  wanakakiliwa na changamoto  mbalimbali

Ambazo alizitakuwa ni ukosefu wa usafiri  hari anayo pelekea  kudandia magari ya viongozi wa serikari na wasiasa na kuwafanya wakati mwingine kuandika habari  kama wanavyo taka viongozi

changamoto  nyingine  ni uwezo mdogo wa kiuchumi hari inayo sababisha waandishi washindwe kujiendeleza  kielimu

mkutano huo  ulimteuwa mkuu huyo wa wilaya ya Nkasi  kuwa mlezi  wa chama hicho  na amehaidi kuwa nunulia vifaa vya awali kwa ajiri ya kuanzisha gazeti la chama hicho  na tayari ameagiza vifaa nchini Marekani

No comments:

Post a Comment