Home » » WAKAZI WA MJI WA MPANDA WAKO HATARAINI KUPATA MAGONJWA YA MLIPUKO‏

WAKAZI WA MJI WA MPANDA WAKO HATARAINI KUPATA MAGONJWA YA MLIPUKO‏


Na Walter Mguluchuma
Mpanda   
Wakazi wa mji wa mpanda  mkoaani  katavi wako hatarini  kupata  magonjwa   ya mlipuko  kutokana  na halimashauri ya mji  huu  kuwalazimisha wafanya biashara wa matunda  kufanyia biashara  katika eneo  lenye  mazingira  machafu.
Wafanyabiashara hao wa matunda   walihamishiwa  na uongozi wa halimashauri  ya mji wa mpanda  kufanyia biashara zao  katika  soko  la zahoro   lilioko  katika  mtaa wa kawajense  kuanzia juzi
Awali   wafanya biashara  hao walikuwa wakifanyi biashara zao  katika   soko kuu la mji huo hadi  hiyo juzi walipo  hamishiwa  kwenye  eneo hilo  ambalo  halikuwa limefanyiwa  maandalizi yoyote  ya  usafi 
Hari hiyo  imewalazimu  wafanyabiashara hao wa matunda ya ndizi  parachichi  nanasi  kuuzia  matunda hayo   chini  kwenye nyasi   kutokana  na soko hilo  kutokuwa na meza  hata moja  za kupangia  matunda  wanayo yauza.
Wakiongea na mwandishi wa habari hizi kwenye   eneo hilo   la soko  wafanya biashara  walieleza  kuwa  hari ya  eneo hilo  ni mbaya mno  kiafya kutokana  na baadhi ya  maeneo  hayo  kutapakaa kwa vinyesi vya binadamu .
Pamoja  na hari hiyo  inawalazimu  matunda  yao   kuyarundika  chini ya  nyasi  matunda hayo  huko  hawajuwi  kama  chini  kuna  uchafu gani .
 Walieza  pia  kuwa aneo  hilo walilo hahamishiwa    halina  huduma yoyote  ya choo  hari ambayo  imekuwa ikiwafanya  wafanya  biashara  wenye watoto wadogo     kutawanya ovyo vinyesi vya watoto wao  katika eneo  hilo  mara wanapo maliza kujisaidia.
Nae  mwenyekiti wa halimashauri ya mji wa mpanda  Enock Gwambasa  akizungumza  na wafanya biashara alipofika  kuangalia   eneo  hilo alisema  amesikitishwa  na uamuzi wa kuwahamishia  wafanya biashara katika   eneo hilo   lenye mazingira machafu.
 Alisema  ameshangazwa  na eneo hilo kuwa katika mazingira  hayo   kwani baraza lake la  madiwani lilimwagiza Mkurugenzi  mtendaji wa  halmashauri  hiyo  miezi 13 iliyo  pita  kutengeneza miundo  mbinu  katika soko  hilo  na  kukisha kamilika  ndiyo   wafanya biashara  wahamishiwe  hapo.
Alifafanua kuwa   inakuwaje  watu wanahamishiwa  kwenye eneo  kama  hilo   hiyvo  atahakikisha  analipatia  ufumbuzi  tatizo hili mapema  iwezekanavyo  ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko   hasa hiki kipindi  cha mvua za  masika.
Kwa  upande wake  Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa mpanda  Joseph  Mchina  alisema  kuwa   sio jukumu la halimashauri yake   kuwatengenezea   miundo  mbinu  wafanyabiashara hao.
Alisema  jukumu lao   kama halimashauri ya mji  ni kuwapatia tuu eneo la kufanyanyia  biashara zao  na si vinginevyo.
 Nae   afisa afya wa  halimashauri ya mji wa mpanda  Patick Kweya  alisema kuwa yeye kama afisa  afya  hajapewa  taarifa yoyote ya kuhamishwa  kwa wafanyabiashara katika eneo  hilo.
Kuanzia  jana wafanya biashara hao  wamegoma kulipia ushuru  kwa kile walicho  dai  eneo    halifai kibiashara  hari  iliyo pelekea polisi kufika katika eneo hilo   lakini waliendelea  na msimamo huo huo wa kugoma  kulipia ushuru wa soko.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa