Na Walter Mguluchuma
Mpanda
Wakazi wa mji wa mpanda mkoaani katavi wako hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kutokana na halimashauri ya mji huu kuwalazimisha wafanya biashara wa matunda kufanyia biashara katika eneo lenye mazingira machafu.
Wafanyabiashara hao wa matunda walihamishiwa na uongozi wa halimashauri ya mji wa mpanda kufanyia biashara zao katika soko la zahoro lilioko katika mtaa wa kawajense kuanzia juzi
Awali wafanya biashara hao walikuwa wakifanyi biashara zao katika soko kuu la mji huo hadi hiyo juzi walipo hamishiwa kwenye eneo hilo ambalo halikuwa limefanyiwa maandalizi yoyote ya usafi
Hari hiyo imewalazimu wafanyabiashara hao wa matunda ya ndizi parachichi nanasi kuuzia matunda hayo chini kwenye nyasi kutokana na soko hilo kutokuwa na meza hata moja za kupangia matunda wanayo yauza.
Wakiongea na mwandishi wa habari hizi kwenye eneo hilo la soko wafanya biashara walieleza kuwa hari ya eneo hilo ni mbaya mno kiafya kutokana na baadhi ya maeneo hayo kutapakaa kwa vinyesi vya binadamu .
Pamoja na hari hiyo inawalazimu matunda yao kuyarundika chini ya nyasi matunda hayo huko hawajuwi kama chini kuna uchafu gani .
Walieza pia kuwa aneo hilo walilo hahamishiwa halina huduma yoyote ya choo hari ambayo imekuwa ikiwafanya wafanya biashara wenye watoto wadogo kutawanya ovyo vinyesi vya watoto wao katika eneo hilo mara wanapo maliza kujisaidia.
Nae mwenyekiti wa halimashauri ya mji wa mpanda Enock Gwambasa akizungumza na wafanya biashara alipofika kuangalia eneo hilo alisema amesikitishwa na uamuzi wa kuwahamishia wafanya biashara katika eneo hilo lenye mazingira machafu.
Alisema ameshangazwa na eneo hilo kuwa katika mazingira hayo kwani baraza lake la madiwani lilimwagiza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo miezi 13 iliyo pita kutengeneza miundo mbinu katika soko hilo na kukisha kamilika ndiyo wafanya biashara wahamishiwe hapo.
Alifafanua kuwa inakuwaje watu wanahamishiwa kwenye eneo kama hilo hiyvo atahakikisha analipatia ufumbuzi tatizo hili mapema iwezekanavyo ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko hasa hiki kipindi cha mvua za masika.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa mpanda Joseph Mchina alisema kuwa sio jukumu la halimashauri yake kuwatengenezea miundo mbinu wafanyabiashara hao.
Alisema jukumu lao kama halimashauri ya mji ni kuwapatia tuu eneo la kufanyanyia biashara zao na si vinginevyo.
Nae afisa afya wa halimashauri ya mji wa mpanda Patick Kweya alisema kuwa yeye kama afisa afya hajapewa taarifa yoyote ya kuhamishwa kwa wafanyabiashara katika eneo hilo.
Kuanzia jana wafanya biashara hao wamegoma kulipia ushuru kwa kile walicho dai eneo halifai kibiashara hari iliyo pelekea polisi kufika katika eneo hilo lakini waliendelea na msimamo huo huo wa kugoma kulipia ushuru wa soko.
No comments:
Post a Comment