Na Walter Mguluchuma, Mpanda-Katavi Yetu
Wajumbe wa tume ya kupokea maoni ya marekebisho ya katiba wamemaliza kufanya mikutano yao katika wilaya ya mpanda jana na wameanza mikutano katika Wilaya ya Mlele itakayo malizika septemba 27 mwaka.
Kamati hiyo yenye wajumbe wanne wakiongozwa na mwenyekiti Mohamed Yusuph Mshamba imemaliza mikutano yake iliyochukua muda wa wiki mbili na kukutana na changamoto mbalimbali ambazo wameomba zirekebishwe kwenye maeneo mengine.
Hayo yalisemwa na na wajumbe wa kamati wakati hiyo walipo kuwa wakizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Lyambalyamfipa mjini mpanda walipo kuwa wakitoa majumuisho ya mikutano yao walio ifanya kakika wilaya ya mpanda .
Mwenyekiti wa tume ya wajumbe hao wanne alitaja baadhi ya changamoto kuwani wananchi hawaku hamasishwa vya kutosha na hali hiyo imesababisha mahudhurio ya watu kuwa ni wachache kwenye mikutano.
Alieleza katika mikutano walio fanya Wilayani Mpanda ni eneo moja tuu la kata ya ikola ndiko waliko jitokeza watu 400 na walishangazwa na mahudhurio ya wananchi wa kata ya mishamo ambapo kwenye mkutano wao kulikuwa na watu tisa tuu.
Changamoto nyingine ni kutojitokeza kwa wanaweke kwenye mikutano ya kupokea maoni ya marekebisho ya katiba na hao wachache wanao jitokeza wamekuwa hawachangii maoni yao.
Alisema pamoja na uchache wa watu kwenye mikutano hiyo wameweza kupata maoni mazuri ambayo yatasaidia kutengeneza katiba.
Nae mratibu wa tume hiyo Haji Omary haji aliwaomba wana siasa na viongozi wa taasisi mbalimbali waache tabia ya kutuma watu wapeleke maoni yao hivyo amewataka wajitokeze wao wenyewe.
Wajumbe wa tume hiyo jana walifanya mkutano wa wa kwanza wilayani mlele katika kata ya kasokola tarafa ya nsimbo na wameanza leo mikutano ya siku sita katika tarafa ya mpimbwe.
Blogzamkioa
0 comments:
Post a Comment