Tuesday, September 11, 2012

TUME YA KUPOKEA MAONI YA KUREKEBISHA KATIBA YALIA NA WANAWAKE MPANDA KUTOJITOKEZA KUTOA MAONI

Na Walter Mguluchuma, Mpanda-Katavi Yetu

Wajumbe wa tume ya kupokea maoni ya marekebisho  ya katiba wamemaliza kufanya mikutano yao katika wilaya ya mpanda jana na wameanza mikutano katika Wilaya ya Mlele  itakayo malizika septemba 27 mwaka.

Kamati hiyo yenye wajumbe wanne wakiongozwa na mwenyekiti  Mohamed  Yusuph  Mshamba imemaliza mikutano yake iliyochukua muda wa wiki mbili  na kukutana na changamoto mbalimbali ambazo wameomba zirekebishwe kwenye maeneo mengine.

Hayo yalisemwa na na wajumbe wa kamati  wakati  hiyo walipo kuwa wakizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Lyambalyamfipa mjini mpanda walipo kuwa wakitoa majumuisho ya mikutano yao walio ifanya kakika wilaya ya mpanda  .
Mwenyekiti  wa tume ya wajumbe hao  wanne   alitaja baadhi ya changamoto kuwani  wananchi hawaku hamasishwa vya kutosha na hali hiyo imesababisha mahudhurio ya watu kuwa ni wachache kwenye mikutano.

Alieleza  katika mikutano  walio fanya Wilayani Mpanda  ni eneo moja tuu la kata ya ikola ndiko waliko jitokeza watu 400  na walishangazwa  na mahudhurio ya wananchi wa kata ya mishamo ambapo kwenye mkutano wao kulikuwa na watu tisa tuu.

Changamoto nyingine ni kutojitokeza kwa wanaweke kwenye mikutano ya kupokea maoni ya marekebisho ya katiba na hao wachache wanao jitokeza wamekuwa hawachangii maoni yao.

 Alisema pamoja na uchache  wa watu kwenye mikutano hiyo wameweza kupata maoni mazuri ambayo yatasaidia kutengeneza katiba.

Nae mratibu wa tume hiyo  Haji  Omary haji aliwaomba wana siasa na viongozi  wa taasisi mbalimbali waache tabia ya kutuma watu wapeleke maoni yao hivyo amewataka wajitokeze wao wenyewe.

 Wajumbe wa tume hiyo jana walifanya mkutano wa wa kwanza wilayani mlele katika kata ya kasokola tarafa ya nsimbo na wameanza leo mikutano ya siku sita katika tarafa ya mpimbwe.
Blogzamkioa

No comments:

Post a Comment