Tuesday, September 11, 2012

MPANDA YAKABILIWA NA TATIZO LA MAJI

Na walter Mguluchuma, Katavi Yetu
Mji wa Mpanda mkoani Katavi unakabiliwa na tatizo la maji kwa kipindi cha zaidi ya wiki moja sasa kutokana na mamlaka ya maji taka na maji safi ya Halmashauri ya mji huo  kukatiwa umeme na shirika la umeme baada ya kushindwa  kulipa bili ya umeme
Hali hiyo imesababisha kupanda kwa gharama ya maisha ya wakazi wa mji wa mpanda wa kufutia kuongezeka kwa kwa bei ya maji katika mitaa mbalimbili ya mji huo 
Kukosekana kwa maji kumesabisha ndoo moja kupanda kwa bei ambapo ndoo moja ya maji inauzwa kwa shilingi mia tano tofauti na hapo awali ndoo moja ilikuwa ikiuzwa kwa bei ya shilingi mia tatu
Meneja wa mamlaka ya maji safi na maji taka wa halmashauri ya mji wa mpanda  Galus Kasonso alisema tatizo hili limetokana na mamlaka ya maji taka na maji safi kushindwa kulipa bili ya umeme
Alisema mji wa mpanda unategemea maji yanayo toka katika bwawa la milala na yanasukumwa na pampu ya mashine na wananchi wengine wanapata maji ya kutengwa yanayo toka kwenye mto manga
Alifafanua kuwa wakazi wa mji wa mpanda wanao athirika na ukosefu wa maji niwale ambao wanategemea maji yanayotoka katika bwawa la milala
Hata hivyo alieleza kuwa tatizo hilo la ukosefu wa maji linategemea kumalizika wiki hii  kwani wanatemea
Blogzamikoa

No comments:

Post a Comment