Home » » NAIBU WAZIRI ATOA AGIZO LA KUCHUKULIWA HATUA WALIMU WANAOFANYA MAPENZI NA WANAFUNZI WAO KWA KISINGIZIO KUWA NDIO RUZUKU YAO YA KUWAFUNDISHIA.

NAIBU WAZIRI ATOA AGIZO LA KUCHUKULIWA HATUA WALIMU WANAOFANYA MAPENZI NA WANAFUNZI WAO KWA KISINGIZIO KUWA NDIO RUZUKU YAO YA KUWAFUNDISHIA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 


Na Walter   Mguluchuma .
      Katavi
NAIBU Waziri  wa  nchi Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) , George Joseph Kakunda ameuagiza uongozi wa Serikali ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi  kuwachukulia hatua kali ya kinidhamu na kijinai mara moja  ikiwemo kuwafukuza kazi walimu wanaofanya mapenzi na wanafunzi wao wa kike .
Naibu Waziri alielezwa  kuwa walimu hao wamekuwa wakidai kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wao  ni sehemu  ya  ruzuku yao ya ualimu
Kufuatia tabia hizo za walimu hao Kakunda alitoa agizo hilo  kwa viongozi wa Serikali ya Wilaya ya Mpanda alipokuwa akizungumza na madiwani na watumishi  wa Halmashauri ya Nsimbo akiwa katika ziara ya  kikazi ya siku moja katika mkoa wa Katavi .
Awali kabla agizo hilo  halijatolewa , Diwani wa kata ya Katumba , Seneta Baraka alimweleza Naibu Waziri  Kakunda kuwa maisha yake yako hatarini kutokana na kuwafuatilia kwa karibu walimu walio na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wao wa kike .
Aliongeza kuwa  baadhi ya walimu wanaofundisha katika shule mbili za sekondari za Katumba na Kenswa  zilizopo katika makazi ya wakimbizi  ya Katumba  wamekubuhu katika kufanya mapenzi na wanafunzi wao wa kike huku wengine wakiwa wamewaoa wanafunzi wao wakiwa bado hawajamaliza masomo yao .
“Baadhi ya walimu wanadai kuwa kufanya mapenzi na wanafunzi wao  ni sehemu ya ruzuku yao ya ualimu ….. nimekuwa nikipata ushirikiano hafifu na uongozi wa wilaya  licha ya kutoa taarifa kwao zinazohusu tabia hizo za walimu hao
Hata hivyo uongozi wa wilaya umeshindwa kuwachukulia walimu hao hatua za kinidhamu na kijinai  licha ya kuwepo ushahidi wa kutosha Badala yake nimekuwa nikitishiwa maisha “ alisema.
Alimweleza Naibu waziri kuwa yupo mwalimu mmoja anayefundisha kati ta shule hizo mbili za sekondari ambaye ameamua kumuoa mwanafunzi wake wa kike ambaye amelazimika kukatiza masomo yake .
“Nilishatoa taarifa ya mwalimu  huyu na wengine  wenye mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wao wa kike  katika vikao vya baraza la madiwani  lakini hakuna  hatua yeyote  iliyochukuliwa dhidi yake  baada yake baadhi ya madiwani  wenzangu  wamevujisha siri za vikao  na kwenda  kuwataarifu  walimu hao kuwa mimi ndio ninaye washtakia” alieleza .

Alieleza kuwa  mwalimu huyo baada ya penzi na mwanafunzi wake wa kike kukolea aliamua kuishi  kinyumba  na mwanafunzi huyo  hadi sasa ambapo tayari ameshalipa mahari  kwa wazazi  wa msichana huyo .
Alisema kuwa hata hivyo mama mzazi wa msichana huyo amekataa katakata kupokea posa ya mwalimu huyo .

 .Alimuomba Naibu Waziri amsaidie ili aweze kupatiwa ulinzi wa kutosha kwa kuwa maisha yake yako hatarini  kutokana na vitisho anayopewa  kwamba hata siku hizi amelazimika kupunguza kutembelea maeneo ya starehe  akihofia  maisha yake .
Mara  baada ya    kupokea  maelezo  hayo  Naibu  Waziri  Kakunda   aliungiza uongozi wa  Serikali ya  Wilaya ya  Mpanda  kuhakikisha inawachukulia  hatua   kari  ikiwemo kuwafukuza kazi walimu wote watakao bainika kufanya  mapenzi na wanafunzi kwa kisingizio  kuwa  ndio ruzuku yao walimu kufanya mapenzi na walimu.
 Alisema sheria  inakaza  mtu kufanya mapenzi  na    mtoto  mwenye umri  chini ya miaka 18 hivyo wanaofanya hivyo watambue kuwa wanafanya  makosa  na wala  hakuna  mtu kusingizia kuwa  wlikubaliana .

Kakunda  alisema lengo la  Serikali ni  kuhakikisha  mtoto  anasoma  kuanzia  darasa la  kwanza   hadi kidato cha  nne  hivyo  aliwaonya wanaowaozesha wanafunzi wakae  chonjo  kwani kufanya hivyo ni kosa kubwa .

 Alizitaka  kamati za ulinzi na usalama za   Kata  hapa  nchini zishirikiane  kufanya kazi ya  kuhakikisha  zinadhibiti  mimba za  wanafunzi kwenye  kata  zao .
Afisa  Elimu wa   Sekondari wa  Halmashauri ya  Nsimbo  Said   Malamba  alisema   baadhi ya  walimu wanaotuhumiwa  kufanya  mapenzi na wanafunzi wao  tayari wameisha  anza kulishughulikia.

 Alisema  na  tayari walimu wawili   wawili wa   shule  ya  Sekondari   Katumba na mmoja  wa   Seokndari ya  Kenswa  walishaandikiwa  barua   na   tume ya utumishi ya kujieleza  kutoka na tuhuma  hizo na  baada ya kujieleza   tayari    Mwalimu  Mmoja  wa  Shule ya  Msingi  Katumba   Mwalimu    Fransis  Manyala   amechukuliwa  hatua  na  walimu  wawili  hawakupatikana  na  hatia.
Alisema  mwalimu  huyo   aliyepatikana  na  hatia  kwenye  tume ya utumishi ya  Wilaya ya  Mpanda   amekata  rufaa  kwenye  tume ya utumishi ya  Taifa  baada ya kutoridhika na maamuzi ya  kusimamishwa  kwake  kazi .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa