Home » » POLISI JELA MIAKA MITATU KWA KUPOKEA RUSHWA YA LAKI SABA .

POLISI JELA MIAKA MITATU KWA KUPOKEA RUSHWA YA LAKI SABA .

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


Na   Walter   Mguluchuma .
        
 Askaari  Polisi   Konsitebo    Peter  Kashuta  wa   kituo  cha  Polisi   Mwese   Wilaya  ya   Tanganyika   Mkoani    Katavi   amehukumiwa  kifungo cha  miaka  mitatu   jela  au  kulipa   faini ya   sh   laki   tano   baada  ya  kuapatikana   na  hatia  ya  kuomba     na  kupokea   Rushwa ya  SHS 700,000 .
    Mshitakiwa  huyo  alihukumiwa  jana   katika   Mahakama  ya   Wilaya  ya   Mpanda   mbele  ya  Hakimu  mfawidhi  wa   Mahakama ya  Wilaya  ya   Mpanda Chiganga   Ntengwa    baada ya   Mahakama  kuridhika  na  ushahidi  uliotolewa    Mahamani  hapo  na   upande wa  mashitaka  uliongozwa  na   wanasheria wa   TAKUKURU    Bahati  Haule  na  Simon  Buchwa .
Hakimu   Ntengwa  kabla  ya  kusoma  hukumu  hiyo  alisema   kutokana  na  ushahidi  uliotplewa   mahakamani  hapo  na  upande   wa  mashitaka  ulikuwa  na  mashahidi  wanane  na  mshitakiwa   hakuwa  na   shahidi    hata  mmoja   Mahakama  iliridhika  na  ushahidi  wa  vielelezo   vilivyotolewa   Mahakamani  hapo  fedha  za  mtego  na   jelada  la  kesi   aliokuwa  akiichunguza mshitakiwa  kama  ushahidi  katika  kesi hiyo.
 Alisema  pamoja  na  mshitakiwa  Peter  Kashuta  kujitetea  kuwa   wakati   anakamatwa  na  maafisa  wa   TAKUKURU  yeye   hakuna  na  pesa  yoyote   ili  aliyokutwa   nayo .
Chiganga  aliendelea  kusoma  hukumu  na  kueleza  kuwa   Mahakama  imeona  kuwa   kitendo  cha   mshitakiwa  kukimbia  na  kisha   kuanza  kupigana  na   maafisa wa  TAKUKURU   kwa  kipindi   kirefu na  baada ya  kuzidiwa   aliamua  kuzitupa   fedha  hizo   ilikuwa  ni   vigumu kuweza  kushika  nazo   fedha  zikiwa   mfukoni  wala  mkononi  kwani  alikuwa    ameisha  zitupa .
  Alisema  ushahidi  mwingine  uliomtia  hatiani  mshitakiwa   atiani  ni  kitendo  cha  kufuata  mshitakiwa  Hotelini   ambae  alikuwa   amepanga   nae  ili  wakabidhiane  kiasi  hicho  cha   fedha  ili   aweze  kumsaidia   kwenye  kesi yake .
Akitowa  adhabu hiyo    Hakimu  Ntengwa   alisema   Mahakama  imemtia  hatiani  mshitakiwa  kwa  kosa  la  kifungu  cha   sheria   Namba  15  cha  sheria ya  kupambana  na kuzuia  rushwa    sura  ya  11 ya  mwaka  2007.
Hivyo  kutokana na  makosa  hayo  mawili  ya kuomba  na  kupokea   Rushwa     kwenda  sambamba   Mahakama  imemsamehe  kwa  kosa  la  kuomba   Rushwa  ila  imemuhukumu kwa  kosa  la  kupokea  Rushwa  hivyo  mshitakiwa   Peter  Kashuta  mahakama   imemuhukumu  kifungo cha  miaka  mitatu  jela   au  kulipa   faini ya Tshs  500,000.
 Awali  katika  kesi  hiyo   waendesha  mashita  wanasheria  wa  TAKUKURU  Bahati  Haule  na  Simon   Buchwa  walidai   mahakamani  hapo kuwa   mshitakiwa   alitenda  kosa  hilo  hapo   Februari  9  mwaka  jana  huko  katika   Kijiji   cha   Mwese   Wilaya  ya   Tanganyika .
Siku  hiyo   mshitakiwa  alidaiwa  kuomba   Rushwa   ya  Tshs  700,000   kutoka  kwa   Luchega   Mambalu    ambae   alikuwa    amefunguliwa  kesi katika  kituo  cha  polisi  Mwese  hata  hivyo   Luchega aliamua   kwenda  kutowa  taarifa  Takukuru  na  ndipo   walipoandaa  mtego  na  kufanikiwa kumkamata  mshitakiwa  Peter  siku  hiyo.
  Hata  hivyo  mshitakiwa  aliweza  kuponyoka  kwenda   kutumikia  kifungo  jela   baada  ya  kulipa    faini ya  shilingi    laki   tano    na  kuweza  kuwa  huru.
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa