Walter Mguluchuma Na Arine Temu
Katavi .
Kaimu Muhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi Elias Manase ametowa rai kwa Watanzania wajenge utamaduni wa kutemmbelea Hifadhi za Taifa kwani maeneo hayo ni muhimu sana na waone ni kama sehemu ya maisha yao ya kila siku kwani gharama ya kutembelea Hifadhi ni ndogo ukilinganisha na gharama ya mtu anayotumia kwenye Bar.
Wito huo aliutowa hapo jana wakati alipokuwa akizungumza na Wandishi wa Habari wa Chama cha Wandishi wa Habari Mkoa wa Katavi waliotembelea Hifadhi ya Taifa ya Katavi .
Alisema pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Katavi kuwa na wanyama adimu bado idadi ya Watalii wa ndani na wanje wanaofika kutembelea Hifadhi hiyo ni wachache .
Hifadhi hiyo ambayo ni miongoni mwa Hifadhi 16 zilizopo hapa nchini ni ya tatu kwa ukubwa ikiwa inazifuatia Hifadhi za Ruaha na Serengeti .
Alisema hifadhi hiyo ina makundi ya Wanyama wengi adimu kama vile makundi makubwa ya viboko na Mbwa mwitu na wanyama wengine aina ya kudu na maporomoko ya maji
Alifafanua kuwa pamoja na kuwepo na vivutio hivyo idadi ya watalii bado halidhishi ingawa kunaongezeko la watalii tofauti na hapo awali .
Manase alisema Hifadhi ya Katavi inakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazoikabili Hifadhi hiyo ya Taifa ilianzishwa rasmi mwaka 1974.
Alizitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni ujangili , uingizwaji wa mifugo ndani ya Hifadhi na kupakana na kambi za Wakimbizi ambapo watu wanao ishi kwenye kambi hizo wamekuwa wakiingiza silaha kutoka nchi jirani na kufanya ujangili ndani ya Hifadhi .
Changamoto nyingine ni miundo mbinu ya barabara pamoja na uchache wa Hotel za kulala Watalii ndani ya Hifadhi na nje ya Hifadhi .
MWISHO
.
0 comments:
Post a Comment