Na Walter Mguluchuma.
Katavi
WAKAZI watatu wa kitongoji cha Senta ya Maradona , kijiji cha
Kabange wilaya mpya ya Tanganyika mkoani Katavi wamekufa baada ya
kunywa dawa ya kienyeji waliyopewa na mganga wa kienyeji aitwae
Msajigwa Jaheda (55) ili kutibu magonjwa ya tumbo ..
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Katavi , Damas Nyanda amewataja
marehemu hao kuwa ni pamoja na Kabula Joseph (23) ambao ni wake
wa mtoto mdogo na mtoto mkubwa wa mganga huyo wa kienyeji ,
mwingine ni Idulu Masanja (30).
Kamanda Nyanda alieleza kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 13 , mwaka
huu saa nne usiku katika kitongoji cha Senta ya Maradona , kijiji
cha Kabange , Kata ya Sibwesa katika wilayani mpya ya Tanganyika
mkoani humo .
Aliongeza kuwa mganga huyo wa kienyeji anatafutwa na polisi ambapo
alitoroka na kujificha kusikojulikana baada ya kutenda uhalifu huo
.
Akisimulia tukio hilo , Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa ya Mpanda , Dk
Mohamed Mpunja ambaye alienda eneo hilo la tukio alisema kuwa
alisema usiku huo wa tukio mganga huyo wa kienyeji alimpatia
mke wa mtoto wake mdogo aitwae Kabula dawa ya kienyeji ya
kusafisha tumbo .
Aliongeza kuwa baada ya kunywa dawa hiyo, Kabula alianza kutapika
na kupoteza nguvu mwili hatimae akafikwa na umauti .
“Mganga huyo alimpatia mke wa mtoto wake mkubwa , aitwae Ndalo
dawa ya kienyeji ya kusafisha tumbo mara baada ya kunywa alianza
kuharisha na hatimae akafriki dunia “ alieleza .
Dk Mpunja alieleza kuwa mtu mwingine aliyepoteza maisha ni
Masanja ambae alifika katika kitongoji hicho kuhani msiba ambapo
kabla ya kurudi nyumbani kwake alienda kwa mganga wa kienyeji ,
Jaheda ili aitibiwe tumbo la ngiri .
“Mganga huyo wa kienyeji alimpatia Masanja dawa ya kienyeji
ambayo aliinywa ndipo akanza kutapika na kuharisha , alifariki
dunia muda mfupi baadae “ alieleza .
Dk Mpunja amewataka wakazi mkoani humo wakihisi dalili za
ugonjwa waende kwenye vituo vya afya vinavyotoa huduma kwa
matibabu huku akiwataka waganga wa kienyeji hususani wa tiba
mbadala wajisajili .
Mwisho
0 comments:
Post a Comment