Home » » MANISPAA YA MPANDA WAHIDI KUONGOZA TENA KITAIFA KWA UFAULU WA WANAFUNZI KATIKA MTIHANI WA RASABA 2017.

MANISPAA YA MPANDA WAHIDI KUONGOZA TENA KITAIFA KWA UFAULU WA WANAFUNZI KATIKA MTIHANI WA RASABA 2017.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

    Na  Walter   Mguluchuma .
            Katavi .
Manispaa ya  Mpanda   Mkoa wa   Katavi   ambayo  imeongoza  Kitaifa  kwa  matokeo ya jumla  ya  ufaulu wa   Wanafunzi    kwa   2016 waliomaliza   darasa la  saba kwa  Manispaa   zote  zilizopo   Nchini  wamedai  kuwa  wataongoza   tena   matokeo ya  ufaulu kwa  mwaka 2017 kwasababu   uwezo wa kufanya  hivyo  wanao .
Kauli  hiyo  ilitolewa  hapo   jana   na  Afisa    Elimu  wa  Manispaa ya  Mpanda  Vicent   Kayombo  wakati   alipokuwa    akiwahutubia   wananchi kwenye  mkutano  wa  hadhara  uliofanyika  jana  kwenye   eneo la   Maridadi   Kata ya  Majengo mkutano  huo  uliokuwa   umeandaliwa  na   Diwani  wa  Kataya  ya   Majengo   Willy  Mbogo  ambae  pia  ni  Meya wa  Manispaa  ya   Mpanda .
Alisema  katika   matokeo ya ufaulu  wa   Wanafunzi   katika  mtihani wa   Taifa  wa  kumaliza      darasa  la   saba  kwa  matokeo   ya  jumla  yaliyotangazwa   hivi    karibuni  Manispaa  hiyo  imeshika  nafasi ya kwanza     kwa  Manispaa   zote   zilizopo  hapa    nchini.
  Manispaa  hiyo  imeweza  kushita   nafasi ya  kwanza  kwa  kipindi cha  miaka   mitatu  mfululizo  ambapo  ilipoongoza  kwa  mara ya  kwanza wapo   watu walisema  wamebahatisha  na  baada ya  matokeo yaliofuata   Halmashauri  nyingi   zimekuja  kujifundisha  kwenye   Halmashauri  hii.
Kayombo  alieleza  kuwa   Manispaa  ya  Mpanda   itaongoza    tena  kwa  ufaulu wa   wanafunzi  watakao  kufanya   mtihani wa  Taifa  wa kumaliza    darasa la   saba.kwa  mwaka   2017 kwa  kuwa  uwezo wa  kufanya  hivyo  wanao  kwa  kuwa  wazazi  wapo , wadau  wapo  na  walimu  wamejipanga  kufanya kazi kweli kweli .
Katika   ufaulu   kwa  mwaka huu  ufaulu  wa    wanafunzi   katika   Manispaa   hiyo  umekuwa  ni   wastani  wa   asilimia 96.5  na wanafunzi   waliofeli  ni   asilimia   3.5 ambapo    shule ya   mwisho  kwa  ufaulu   katika   Manispaa  hiyo  imepata  wastani  wa   asilimia   68  wastani  ambao  ni  ufaulu  kwa   baadhi ya   shule nyingine   hapa    nchini .
 Alifafanua  kuwa jumla  ya    wanafunzi   2116 walifanya   mtihani wa  Taifa  wa  kumaliza   darasa  la  saba   ambapo  wanafunzi   2045 wamefaulu  na   71 wamefeli  mtihani kutokana  na  kuwa  watoro .
Alitaja  ufaulu kwa  kipindi  cha   miaka   mitatu  kwa  manispaa   hiyo  ulikuwa  ni  mwaka   2014  ufaulu  ulikuwa ni  asilimia  90  mwaka  jana  ufaulu  ulikuwa ni   Asilimia    97  na  mwaka huu  ni   asilimia    96.5.
 Alisema miaka  ya  nyumba  watu  walikuwa  wanaidharau  mikoa ya  pembezoni  kuwa   haina   mwamko  wa   elimu   kitu  ambacho  sio  kweli   leo   hii  Mikoa  hiyo  iliyokuwa  ikisema   hivyo  ndio    wanaisoma   namba  kwa  Mkoa wa    Katavi  ambao umeshika   nafasi ya  pili kwa  ufaulu wa   wanafunzi wa  darasa  la  saba kwa  matokeo ya  jumla   katika  mikoa  ya  hapa   nchini .
Mafanikio ya  manispaa  hiyo   na   Mkoa      kufanya   vizuri  katika  ufaulu  kumetokana  na   mwamko wa   elimu walionao  wazazi  na  ushirikiano  wanaoutowa  wazazi kwa  walimu  pamoja  na   mpango   kazi  waliojiwekea  walimu .
Nae   Meya wa   Manispaa ya  Mpanda  Willy  Mbogo      alisema   Manispaa  ya  Mpanda   imepanga   kuchangisha  fedha  kwa   ajiri ya  kuboresha    elimu   ili  wanafunzi   waendelee  kufanya   vizuri  zaidi .
 Alisema   kwa  sasa    hawana  tatizo  la  upungufu  wa   madawati  kwani  hakuna  wanafunzi  wanaosoma  wakiwa  wamekaa   chini  bali   tatizo  lililopo  ni  upungufu  wa  vyumba  vya   madarasa .
Mbogo  alieleza  kwa  sasa   mkakati   uliopo  ni  kuhakikisha  nguzo  zinaelekezwa  katika  ujenzi wa  vyumba  vya   madarasa ,  matundu ya  vyoo  na  nyumba  za  walimu .
 Pia   aliwapongeza walimu  wa   Manispaa  ya    Mpanda   kwa  jitihada   zao  kubwa  wanazofanya  za  kufundisha   wanafunzi   hari   ambayo   imepelekea   kuongezeka  kwa   ufaulu  wa   wanafunzi  wanaomaliza    darasa  la  saba .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa