Home » » HATARI: AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI MBILI KICHWANI NA KIFUANI AKIWA ANAKUNYWA POMBE KWEYE BAR

HATARI: AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI MBILI KICHWANI NA KIFUANI AKIWA ANAKUNYWA POMBE KWEYE BAR


Na  Waller Mguluchuma
Katavi
 Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la  John     Salehe (32) Mkazi wa Kijiji  cha  Itenka  Tarafa ya Nsimbo  Wilaya ya Mlele Mkoani  hapa  ameuwawa kikatili  kwa  kupigwa  risasi  kichwani  na kifuani  na mtu asiye julikana  wakati akiwa anakunywa pombe kwenye baa
Kwa mujibu wa Kamanda wa jeshi la polisi wa Mkoa wa Katavi kamishina  msaidizi mwandamizi Dhahiri Kidavashari tukio hilo la mauwaji ya kinyama  lilitokea hapo juzi kijijini  hapo majira ya saa mbili kamili usiku
 Alisema kabla ya  tukio  hilo marehemu alikuwa  amekaa  akinywa  katika baa moja iliyopo kijijini hapo  inayomilikiwa  na mkazi mmoja wa kijiji  hicho cha Itenka  aitwaye  Mussa Juma(DEO)
 Alieleza marehemu  alifika  kwenye baa  hiyo  toka majira ya saa kumi  na moja jioni  na toka muda huo   aliendelea kunywa   pombe kwenye baa hiyo huku akiwa na baadhi ya watu ambao nao pia walikuwa  wakinywa pombe kwenye baa hiyo ya Mussa Juma ambayo ni maarufu kijijini hapo kwa  kuuza pombe za  iana ya bia mbalimbli
 Ndipo  muuaji huyo asiye fahamika  alifika hapo  na kufyatua risasi mbili  zilizompiga  marehemu  kifuani  na kichwani  na  marehemu alifariki hapo hapo
 Kidavashari  alieleza  kuwa  katika tukio hilo  mtu mmoja  aliyejulikana kwa  jina  la James  Omar(30) Mkazi wa Kijij hicho cha Itenka  ambae nae alikuwa kwenye eneo hilo  alijeruhiwa  kwa kupigwa  na risasi moja  na bunduki  ya aina ya SMG kwenye maeneo ya  kiunoni
 Alisema majirani  wa eneo  hilo i baada ya muda walifika kwenye eneo hilo kwa lengo la kutowa msaada hata hivyo  walikuta  muhusika aliyafanya tukio hilo alikuwa ameisha tokomea mahari  kusiko julikana
Chanzo  cha  tukio  hilo bado  halijajulikana  na wala hakuna mtu wala watu waliokamatwa  kuhusiana na mauwaji ya  hayo ya kikatili ya mtu huyo

 Kamanda Kidavashari alisema  jeshi la Polisi   Mkoaani  Katavi  linaendelea  kufanya msako mkali  ili  kuewza  kuwabaini  na kuwakamata  wale wote waliohusika  katika mauwaji hayo  ili sheria iweze kuchukua mkondo wake
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa