Home » » HALMASHAURI YA MJI KUNUNUA NYUMBA 68 ZA NHC KWA AJIRI YA WATUMISHI WAKE

HALMASHAURI YA MJI KUNUNUA NYUMBA 68 ZA NHC KWA AJIRI YA WATUMISHI WAKE


Na  Walter   Mguluchuma
Katavi
 Halmashauri ya Mji  wa Mpanda Mkoani  Katavi  inatarajia kununua nyumba  68 za  Shirika la  nyumba la Taifa(NHC) kwa ajiri ya kukabiliana na tatizo linalowabili watumishi wake la ukosefu  wa nyumba za kuishi
Haya yalielezwa hapo juzi  kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mjiwa Mpanda  na mwenyekiti wa kamati wa kamati ya  Mipango miji  Ardhi  na Maliasili na mazingira  Wily  Mbogo  alipokuwa akiwasilisha kwenye  Baraza la Madiwani taarifa ya utekelezaji  wa shughuli mbambali za kamati hiyo kwa kipindi cha  miezi  mitatu Julai  hadi Septemba mwaka huu
 Alisema  katika kubaliliana na tatizo la uhaba wa  nyumba za kuishi kwa watumishi wa Halmashauri  hiyo wameamua kuanza kufanya mchakato wa kununua nyumba za 68 za Shirika la Nyumba la Taifa zilizoko katika mtaa wa Ilembo
Mbogo  aliliambia Baraza hilo la madiwani kuwa  Kikao  cha  Baraza la madiwani kilicho kaa hapo Septemba 26 mwaka huu kilimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri  afanye  ulinganisho  wa gharama ya  mkopo  wa kununulia nyumba hizo kwenye  mashirika  na taasisi  za kifedha  mbalimbali
Alieleza  Mkurugenzi  alizingatia  agizo hilo  na  alifanya malinganisho kwenye  taasisi na mashirika ya kifedha mbalimbali kama alivyokuwa  ameagizwa
 Alifafanua  Tanzania   Local  Goverment Loon board liba ya mkopo wao ni  asilimia 26 Banki ya CRDB riba  ya mkopo ni asilimia  18 n,Banki ya NMB  riba yao ya mkopo ni  asilimia 18 na TIB rIba yao  ni asilimia nne
 Baada ya taarifa ya mwenyekiti huyo wa kamati ya  mipango miji   Ardhi na mazingira Baraza hilo lilitowa maamuzi ya kuchukuwa Mkopo kwenye Banki ya  TIB kwa ajiri ya ununuzi wa  nyumba 68 za shirika la nyumba la  Taifa
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashari ya Mji wa Mpanda Enock Gwambasa  alilieleza  baraza hilo kuwa  Halmashauri  itafanya wawasiliano na Wizara ya  ofisi ya Waziri Mkuu(TAMISEMI) kwa ajiri ya  kuwapatia  kibali cha kuchukua  mkopo huo TIB  kama ambavyo taratibu zinavyoelekeza
Alisema Halmashauri hazina mamlaka ya kuingia mikataba ya kukopa fedha kwenye mabanki mpaka wawe wamepewa kibali na TAMISEMI na ndio maana Halmashauri yake itafanya hivyo

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa