Home » » SHIDEFA NET WORK YATOA MSAADA KWA WENYE VVU WA MILIONI 12‏

SHIDEFA NET WORK YATOA MSAADA KWA WENYE VVU WA MILIONI 12‏


Na Walter Mguluchuma 
Mpanda
Blogs za mikoa 
Taasisi isiyo ya kiserikali inayo shughulikia watu wanaoishi na VVU(SHIDEPHA NETWORK) Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi limetoa msaada wavyakula kwa watu wanaoishi na VVU vyenye thamani ya shiligi Milioni 12

Watu hao wanaishi na VVU walikabidhiwa msaada huo hapo jana na mratibu wa SHIDEPHA wilaya ya Mpanda Euzebius Ngurusha.

Ngurusha alisema kuwa jumla ya watu 52 wanaoishi na VVU ndio walio nufaika na msaada huo ambao umetolewa na shirishi la WATERLEED la nchini Marekani.

Katika msaada huo kila ambaye anaishi na VVU ambaye ni mwanachama wa SHIDEPHA NET WORK alikabidhiwa kilo 80 za mahindi na maharage debe mbili.

Alitaja msaada mwingine waliopewa kuwa ni mchereme kilo 5, Sukari kilo 5 pamoja na sabuni za kufulia miche 4 kwa kila mwanachama ambao misaada hiyo imegharimu jumla ya shilingi 12,400,000/= za kitanzania.

Alisema watu wanaoishi na VVU wilayani mpanda ambao ni wanachama wa SHIDEPHA NET WORK wamekuwa wakinufaika na msaada unaotolewa na shirika hilo la WSTERLEED la nchini Marekani toka mwaka 2008 shirika hilo lilipoanza kutoa misaada.

Ngurusha alifafanua kuwa SHIDEPHA NET WORK mbali ya kutoa misaada hiyo kwa wanachama wake pia inatowa huduma kwa watoto yatima wanaoishi mitaani.

Pia wanaotowa elimu kwa wanachama wao wanaishi na VVU ya ujasiliamali kwa wale waliopata afya ili waweze kujikimu kimaisha.

Aidha shirika hilo linatowa msaada kwa wanafunzi wa shule za misingi na sekondari ambao wazazi wao wamefariki dunia kwa kuwalipia ada na kuwanunulia sare za shule.

Mmoja wa watu wanaoishi na VVU Tausi Maulod (40) mkazi wa mtaa wa Nsemulwa alilishukuru shirika hilo kwa msaada huo ambao utaweza kuwasaidia kupandisha CDFOR zao.

Pia aliwashauri wananchi waache tabia ya kuogopa kupima afya zao mara kwa mara ili watakapo bainika kuwa wana VVU itawasaidfia kujitambua na wataweza kuwaokoa watu wengine kwa kuwa tayari watakuwa wameishajitambua.

1 comments:

Unknown said...

NASHUKURU KWA KUA MASHIRIKA MBALIMBALI YANAWAJALI WAHITAJI. NIOMBE SAPOTI MAANA NINA MUDA MLEFU NIMEANZISHA SHIRIKA LA KUWASAIDIA WALEMAVU NA WATOTO WAO KUPATA ELIMU ILA KASI NI KIDOGO HUKU MAHITAJI NI MAKUBWA NIOMBE KAMA KUNA MTU AU WATU WEMA WA KUNISAPOTI KUTEKELEZA HILO NITAFURAHI NAkama kuna ushauli wasiliana nasi kwa"wheelchairfoundationtanzania@gmail.com

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa