Mkazi wa Kijiji cha Uluila Wilaya Mlele Mkoa wa Katavi Jonathani Laftari akiwa katika kituo cha polisi cha Mkua wa katavi alipokuwa akihojiwa baada ya kukamatwa na bunduki aina ya SMG yenye namba M22-13350 ikiwa na risasi 37 akiwa chini ya ulinzi wa afisa upelelezi wa makosa ya jinai wa Mkoa wa Katavi kulia kwake.
Bunduki ya kivita aina ya SMG yenye namba M22-13350 ikiwa na risasi 37 pamoja na panga na kisu alivyo kamatwa navyo jonathani laftari (26) Mkazi wa Kijiji cha Uluila Wilaya Mlele Mkoa wa Katavi kufuatia msako mkali uliofanywa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na askari wa Tanapa.
Askari wa jeshi la polisi pamoja na askari wa Tanapa wa hifadhi ya Katavi wakiwa na mtuhumiwa Jonathani Laftari (mwenye tishet nyekundu) Mkazi wa Kijiji cha Uluila Wilaya Mlele Mkoa wa Katavi walie mkamata na bunduki ya kivita aina ya SMG yenye namba M22-13350 pamoja na risasi 37 ndani ya hifadhi ya mbuga ya katavi.
Na Walter Mguluchuma, Mpanda-Katavi Yetu
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia Jonathani Charles Naftari (26) mkazi wa kijiji cha Uruila baada ya kukamatwa na bunduki ya kivita na risasi 37 ndani ya hifadhi ya Katavi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa habari kuwa mtuhumiwa alikamatwa hapo jana majira ya saa 8:00 mchana katika eneo la Kalumbi ndani ya hifadhi ya Katavi akiwa na Bunduki Sub-Machine Gun (SMG)yenye namba M22 – 13350 pamoja na risasi 37 zikiwa ndani ya magazine yake na risasi nyingine saba zilikuwa ndani ya mfuko wa serikali.
Mtuhumiwa alikamatwa siku hiyo kufuatia msako mkali ambao ulifanywa na askari wa jeshi la polisi kwa kushirikiana na askari wa hifadhi ya katavi
Kidavashari alieleza kuwa mtuhumwa ambaye alikuwa na wenzake watatu walipozungukwa na askari wa polisi na Tanapa na kutakiwa kujisalimisha walikataa kutii amri hiyo na ndipo walipoanza kuwafyatulia askari risasi hovyo kuwalenga askari
Ndipo askari walipojibu mapigo ya risasi na hatimaye majangiri hao walianza kutimua mbio na askari kwa ustadi mkubwa walifanikiwa kumkamata Jonathani na silaha hiyo ya kivita.
Baada ya mtuhumiwa kukamatwa alipekuliwa na kukutwa na risasi saba ndani ya mfuko wa saluari pamoja ana panga na kisu ambacho kilikuwa na damu.
Kamanda Kidavashari alisema mtuhumiwa alipofikishwa katika kituo cha polisi alidai kuwa silaha hiyo ilikuwa ni mali yake na yeye na wenzake waliingia ndani ya hifadhi kwa lengo la kuwinda wanyama.
Kidavashari alieleza polisi kwa kushirikiana na Askari wa Tanapa wanaendelea na msako kuwatafuta watuhumiwa watatu waliotoroka kwenye tukio hilo.
Pindi upelelezi wa tukio hili utakapokamiliaka mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabiri
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment