Na Walter Mguluchuma .
Katavi
Wakala wa Mpango wa wa kuinua ubora wa Elimu kwa shule za msingi Tanzania EQUIP Mkoa wa Katavi umetoa mafunzo kwa Wandishi wa Habari wa Mkoa wa Katavi ya kuwajengea uwezo wa uwelewa wa nanma ya kuielimisha jamii juu ya mpango wa kuinua ubora wa elimu kwa shule za msingi za Mkoa huo..
Mafunzo hayo ya siku mbili yaliowashirikisha Wandishi wa Habari wa vyombo vya habari vilivyopo katika Mkoa huo yalifanguliwa jana katika ukumbi wa idara ya maji na mwakilishi wa Afisa Elimu wa Mkoa wa Katavi John Pandisha ambae pia ni afisa elimu ya watu wazima wa Mkoa wa Katavi .
Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo hayo Pandisha alisema EQUIP Tanzania Wanatambua umuhimu wa wanahabari na ndio maana wameamua kuwapatia mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wa kuelimisha jamii namna bora ya kuinua ubora wa elimu.
Alisema mpango huu wa kuboresha elimu utasaidia kuinua ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi za Mkoa wa Katavi ambapo Mkoa huo umeanza kushuka kwa matokeo ya ufaulu wa wanafumzi wa darasa la saba ambapo kwa mwaka 2015 Mkoa huo uliongoza Kitaifa mwaka 2016 Mkoa ulishiika nafasi ya pili na mwaka jana ufaulu ulishuka na Mkoa ulishika nafasi ya tisa kwa ufaulu Kitaifa .
Alifafanua kuwa mpango huu wa kuboresha elimu utasaidia kupunguza tatizo liliokuwa likiwakabiliwa wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuatia Equip kuamua kujenga shule shikizi kwenye maeneo ambayo wanafunzi wanakaa mbali na shule mama.
Mratibu wa EQUIP Tanzania wa Mkoa wa Katavi Laulent Mpuya alisema mpango huu wa ubora wa kuinua ubora wa elimu na kuongeza ufaulu wa wanafunzi kwa hapa nchini ulianza mwaka 2014 na kwa Mkoa wa Katavi ulianzishwa mwaka jana na kwa sasa upo katika mikoa tisa hapa nchini ,
Alisema Equip katika mpango wa kuinua ubora wa elimu umepanga kujenga madasa kwa ajiri ya shule shikizi kwenye Halmashauri zote tano kwenye maeneo yote ambayo yako mbali na shule mama ilikuwafanya wanafunzi kupata elimu .
Pia wanajenga mapaa ya majengo ya madarasa yaliofikia hatua ya kuenzekwa bati kwenye baadhi ya shule za msingi ambazo wanazokuwa wamezikagua na kujilidhisha kuwa shule hizo zinasitahili kumaliziwa ujenzi na Equip Tanzania .
Mpuya alifafanua kuwa kwa shule shikizi wanatowa kiasi cha Tshs milioni 60 kwa ajiri ya ujenzi wa darasa moja, stoo kwa ajiri ya kutunzia vifaa vya kufundishia na kujifunza pamoja na matundu mawili ya vyoo na kwenye shule mama ambazo zipo kwenye mpango hupewa fedha milioni 12 kwa ajiri ya uwenzekaji wa paa,kupiga bati na ukamilikaji wa jengo la darasa.
Mtaalamu mshauri wa Elimu wa Equip wa Mkoa wa Katavi Semen i Kime alisema mpango huu wa kuboresha elimu unatowa mafunzo kazi kwa walimu wakuu na waratibu kata wa elimu ,
Alisema wamejipanga kuhakikisha wanashirikiana na wadau wengine wa elimu kuongeza ubora wa elimu na kuhakikisha kiwango cha elimu hakishuki tena katika mkoa huu na watahakisha wanaondoa mimba za utotoni kwa kuboresha miundo mbinu ya elimu itakayo wafanya watoto wa kike wasitembee umbali mrefu kwenda kwenye shule wanazo soma .
Semeni alieleza kuwa mpango huo wa kuboresha elimu unaishirikisha jamii husika ili iweze kutambua umuhimu wa ushiriki katika mpango .
No comments:
Post a Comment