MH Seleman Kakoso akipokea msaada wa magodoro yaliotolewa na vitanda na NMB kwa ajiri ya kituo cha Afya Mwese
Kikundi cha ngoma cha kijiji cha Mwese wakitumbuiza wakati wakukabidhiwa msaada wa vitanda
Meneja mausiano wa NMB na Serikali wa Nyanda za Juu Focus
Lubende akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe
Mhando muda mfupi kabla ya kukabidhi msaada wa vitanda viwili vya
kujifungulia akina mama na vitanda vitano vya kulalia wagonjwa
pamoja na magoro yake na seti tatu za vifaa kwa ajiri ya
kufanyia upasuaji vifaa hivyo vilikabidhiwa kwa ajiri ya kituo cha
Afya Mwese Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi
Na Walter Mguluchuma .
Katavi
Benki ya NMB imetowa msaada wa wa vitanda viwili vya kujifungulia akina Mama wajawazito vitanda na vitano vya kulalia wagonjwa vikiwa na magododo vikiwa na na thamani ya Tshs 5.5 kwa ajiri ya kituo cha Afya Mwese kilichoko katika Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi .
Mbali ya vifaa hivyo walivyokabidhi kwa ajiri ya kituo hicho cha Afya kiilichoko umbali wa kilometa 120 kutoka makao makuu ya Mkoa wa Katavi Banki hiyo pia imetowa msaada wa vifaa seti tatu vya kufanyia upasuaji na mashine tatu za kupimia ugonjwa wa moyo kwa ajiri ya kituo hicho cha Afya.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo jana Meneja mausiano wa NMB na Serikali wa Kanda ya Nyanda za juu Focus Lubende alisema msaada walioutowa ni sehemu ya utaratibu ambao Benki hiyo iliyojiwekea wa kutowa faida wanayoipata wameipata sehemu nyingine huwa wanaitowa kwa ajiri ya kusaidia kwenye jamii kila mwaka .
Pamoja na hayo alisema msaada huo wametowa ili kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha huduma za afya na miundo mbinu kuanzia kwenye Zahanati hadi kwenye Hopitali.
Alisema kwa mwaka jana katika sehemu ya faida waliopata kiasi cha Tshs bilioni 16 walizirudisha Serikalini na kiasi cha Tshs Bilioni walitenga kwa ajiri ya kusaidia jamii kama ambavyo walivyofanya kwa kituo cha afya Mwese.
Lubende alieleza kuwa NMB ni Benki ya Serikali na ndio maana imekuwa ikichangia maendeleo ya wananchi kwa kutenga kiasi cha fedha kwa ajiri ya kusaidia jamii na katika Mkoa wa Katavi NMB imekuwa wachangia kwenye elimu na afya .
Aliwataka wananchi kuacha tabia ya kukaa na fedha kwenye mito ya vitanda vyao na badala ya wafungue akaunti Benki kwani kufungua akaunti kuna faida sana kwenye maisha yao .
Aliema NMB inao wateja zaidi ya milioni mbili hapa nchini na wanatarajia kuweka mawakala vijijini kwa ajiri ya watu kupatiwa huduma za Kibanki .
Nae Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando alisema msaada huo waliotowa Nmb inaonyesha jinsi benki hiyo inavyoshirikiana na wanyonge
Aliwasisitiza watumishi wa kituo hicho cha afya kutumia vizuri vifaa hivyo walivyopewa msaada kwa kuvitunza na kuvitumia kwa matumizi yaliokusudiwa kwani Nmb wamefanya jambo kubwa na lahuruma kwa wananchi wa Tarafa ya Mwese.
Mbunge wa Mpanda Vjijijini Moshi Kakoso alisema vifaa hivyo vitasaidia vitaboresha huduma za afya kwenye kituo hicho ambacho ndio kituo kichakavu kuliko vituo vyote vya afya vilivyoko katika Mkoa wa Katavi .
Alisema NMB ni wadau wapekee wanaoangalia jamii kwani wamekuwa wakisaidia Watanzania wote bila kujari kama ni wadau wao au sio wadau wao .
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda iliyoko katika Wilaya ya Tanganyika Malaka Morisho alisema vifaa hivyo walivyopewa watavitunza ili waendelee kuwakumbuka na kuwaenzi NMB.
Kaimu mganga mfawidhi wa kituo hicho cha afya Mwese Masanja Mbogosa alieleza kuwa kituo hicho kilikuwa na changamoto ya upungufu wa vitanda vya kulalia na vya kujifungulia wajawazito .
Alisema vitanda vilivyopo katika kituo hicho ni 19 kati ya hivyo viwili vilikuwa vya kujifungulia akina mama hivyo msaada huo utasaidia kupunguza tatizo la vitanda ambapo pia kituo hicho kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa gari la wagonjwa ,maji ya uhakika na umeme .
No comments:
Post a Comment