Na Walter Mguluchuma .
Katavi
Katika Hali isiyo ya kawaida uongozi wa Chama na Serikali wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi umemwomba Rais John Magufuli kumwacha Wilayani humu kwa muda mrefu Mkuu wa Wilaya Salehe Mhando kutokana na uchapakazi wake mzuri na maendeleo anayoyafanya katika Wilaya ya Tanganyika .
Mhando ndio Mkuu wa Wilaya ya kwanza wa Tanganyika iliyoko katika Mkoa wa Katavi iliyoanzishwa mwaka 2016 na kuwa miongoni mwa wilaya tatu zinazounda mkoa huo.
Akizungumzia ombi hilo wakati wa hafla ya kupokea msaada wa vitanda vya kujifunguliwa akina mama wajawazito na vya kulalia wagonjwa vilivyotolewa na Benki ya NMB kwa ajiri ya kituo cha Afya Mwese iliyofanyika katika kituo hicho cha Afya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpanda iliko Tanganyia Hamad Mapengo alisema ombi hilo wanalitowa kutokana na uchapakazi wake wa Dc huyo,kupenda kwake maendeleo na moyo wake wa kujituma .
Alisema kwa muda aliokaa na kuiongoza Wilaya hiyo kumekuwepo na mabadiliko makubwa ya maendeleo kutokana na usimamizi wa DC huyo utadhani amefanya kazi kwenye Wilaya hiyo wa zaidi ya miaka mingi .
Mapengo alieleza Wilaya hiyo inayovijiji 55 na Kata 16 lakini Mkuu huyo wa Wilaya kwa kupenda watu na kupenda kuwatumikia hakuna sehemu kwenye Wilaya hiyo ambayo haja fika hivyo ni vema Rais Magufuli akamwacha muda mrefu kwenye wilaya ya Tanganyika ilizidi kuwatumikia wananchi na kuwaletea Maendeleo.
Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Moshi Kakoso Dc huyo anawapenda wananchi wake hivyo ni vema apewe ushirikiano na aendelee kufanya kazi kwenye Wilaya hiyo ili izidi kuwa na maendeleo .
AlIsema yeye mwenyewe kama Mbunge wa Jimbo pekee liliko katika Wilaya ya Tanganyika ambalo ameliongoza kwa kipindi cha pili sasa yapo maeneo ambayo kama mbunge hajawahi kufika lakini kwa kipindi kifupi DC huyo amefika na kuonyesha kuwa Dc amekuwa mwenyeji kuliko hata yeye na hiyo inatokana na uchapakazi wake .
Kakoso alieleza yupo tayari kufunga safari kwenda kwenye mamlaka husika ilikuomba ridhaa mkuu huyo wa Wilaya aendelee kufanya kazi kwenye Wilaya ya Tanganyika .
Diwani wa viti maalumu Thiodola Kisese alisema kutokana na utendaji kazi wa Salehe Mhando amekuwa akipewa majina mbalimbali kutokana na maendeleo anayoyafanya kwa kusimamia miradi ya maendeleo kwa karibu .
Alisema wapo wanao mwita mzee wa malu malu hii ni kutokana na usimamizi wake wa majengo ya shule za msingi na sekondari ambapo kuna shule 16 amezisimamia na sasa zina malu malu chini ya sakafuwapo wengine wanamwita maji mdundiko ni kutokana na jitihada zake alizozifanya za kuondoa pampu za maji za kusukumu alizokuwa alizozipa jina bomba mdundiko na sasa wameweka visima vya maji kwenye maeneo ya pampu mdundiko.
MWISHO
No comments:
Post a Comment