Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda amewataka Askari polisi kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi yao na uzalendo ili weweze kuaminiwa na kujijengea shima kwa wananchi.
Kauli hiyo aliitowa hapo jana wakati wa afla ya makabidhiano ya mabati bando 40 yaliotolewa na wadau mbalimbali na Askari kwa ajiri ya ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa mikutano na sherehe iliyofanyika jana katika kantini ya Polisi ya Mkoa wa Katavii .
Alisema ili askari polisi aweze kujijengea heshima kwa watu ni lazima afanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi yake na awe mzalendo na akifanya hivyo jamii yote itakuamini .
Alieleza kuwa jeshi la polisi Mkoa wa Katavi linawashukuru wadau mbalimbali waliochangia mpaka sasa ujenzi wa ukumbi huo ambao umefikia hatua ya kupigwa paa la juu .
Alifafanua kuwa wamepokea jumla ya michango mbalimbali kutoka kwa wadau wa maendeleo na askari polisi ambapo mpaka sasa wamepokea kiasi cha Tshs Milioni 31,221,000.00 katika ya fedha hizo Shilingi milioni 12,129,000 zimechangwa na askari polisi na wadau mbalimbali wa maendeleo wamechangia kiasi cha Tshs Milioni 19,092,000.
Aliwashuru wadau wote waliochangia mchango huo na kuwaomba waendelee na moyo huo na usiwe kwa polisi peke yake bali wafanye na kwenye taasisi nyinnnnnnnnnnngine pia ambazo nazo zinahitaji misaada ya michango kutoka kwa wadau .
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga alieleza kuwa Mkoa wa Katavi unao wadau wengi wa maendeleo na wamekuwa wakichangia kwenye maswala mbalimbali ya maendeleo kwenye jamii kama vile elimu afya na maji .
Nae Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi alisema yeye kama Mbunge hataacha kuwazungumzia askari polisi ndani ya bunge na nje ya bunge juu ya changamoto walionayo askari ya nyumba za makazi ya kuishi .
Alisema Askari polisi wanafanya kazi kubwa sana ya kulinda usalama wa raia na mali zao na jitihada hizo zinaonekana wazi wazi katika Mkoa wa Katavi kwani wameweza kupunguza matukio ya uharifu na ujambazi uliokuwepo mika nyuma katika Mkoa huu hari ambayo ilikuwa ikfanya baadhi ya wafanyabiashara kuhama nyumba zao nyakati za usiku kwa kuhofia kuuawa .
Msimamizi wa mradi huo mratibu wa polisi Kway Ngoroma alisema fedha hizo walizopatiwa watahakikisha wazitumia vizuri na kwa malengo yaliokusudiwa na singinevyo .
Alisema mbali ya mradi huo wa ujenzi wa ukumbi wa mikutano jeshi hilo pia linaendelea na ujenzi wa zahanati ambayo itakapo kamilika itasaidia askari polisi kupatiwa matibabu hapo na jamii ya wakazi wa Manispaa ya Mpanda.
MWISHO
No comments:
Post a Comment