Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma.
Katavi .
Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa TAKUKURU Mkoani Katavi imewakamata Nicodemo Peter na Peter Mwaninsawa wakazi wa Mtaa wa Nsemlwa Manispaa ya Mpanda kwa tuhuma za kupokea Rushwa Wakati wakiwa nje ya jengo la Ikulu ndogo ya Mkoa wa Katavi ya Tshs 400,000 baada ya kuijifanya wao ni maafisa wa TAKUKURU .
Wahumiwa hao wawili walikamatwa hapo jana majira ya saa nne asubuhi wakiwa wanapokea kiasi hicho cha fedha katika eneo la nje ya jengo la Ikulu ndogo ya Mkoa wa Katavi iliyopo jirani na ofisi ya TAKUKURU.
Kamanda wa Takukuru wa Mkoa wa Katavi John Minyenya aliwaambia wandishi wa Habari jana ofisini kwake kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia mtego uliondaliwa na taasisi hiyo baada ya kuwa wamepata taarifa kutoka kwa msiri wao juu ya watu hao waliokuwa wakijiita ni maafisa wa TAKUKURU wa kitengo cha uchunguzi .
Alisema kabla ya kukamatwa kwa wahumiwa hao walimpigia simu msiri wa TAKUKURU na kujitambulisha kuwa wao ni maafisa wa TAKUKURU na wanalo jalada la uchunguzi za huhuma zinazo mkabili msiri huyo .
Hivyo walimtaka awape kiasi cha shilingi laki nne ili waweze kulifunga jalada kwa kufuta tuhuma zilizomkabili msiri huyo ambae ni Mtendaji wa Kijiji cha Vikonge Wilayani Tanganyika ambae walidai kuwa alikuwa na tuhuma za kupokea rushwa ya kutoka kwa wafugaji ambao alikamata mifugo ya wafugaji na kisha aliiachia baada ya kupokea Rushwa kiasi cha Tshs 2,500,000 .
Minyenya alieleza kwa kuwa msiri huyo ambae hapendi na anapinga Rushwa alilazimika kufika kwenye ofisi ya Takukuru na kutowa taarifa juu ya maafisa hao bandia wa Takukuru .
Ndipo Takukuru walipoanza kufanya uchunguzi juu ya malalamiko hayo kutokana na TAKUKURU kutokuwa na watu wenye tabia kama hiyo ya kuomba na kupokea Rushwa .
Alisema ndipo hapo TAKUKURU walipoandaa mtego wa kuwakamata watuhumiwa hao ambao walimtaka msiri huyo awapelekee fedha hizo nje ya jengo la Ikulu ndogo ya Katavi kwa kuwa ni jirani na ofisi yao ya Takukuru ili iwe rahisi wao kutoka ndani ya osisi ya TAKUKURU Na na kufika kwenye eneo la tukio.
Kufuatia makubaliano hayo msiri ulipofika muda wa kupeleka fedha kwa maafisa hao bandia alikwenda kuchukua fedha zilizokuwa na namba za TAKUKURU na kisha aliwapelekea kwenye eneo walilokuwa wamekubaliana kwa ajiri ya kubabidhiana na mara tuu walipo pokea fedha hizo nje ya njengo la Ikulu watuhumiwa hao walikamatwa na Maafisa wa TAKUKURU huku wakiwa na fedha hizo .
Kamanda Minyenya alisema watuhiwa hao wanaendelea kushikiliwa na watafikishwa mahakamani ili wakaweze kujibu mashita mawili ambayo ni kujifanya maafisa wa Takukuru na shitaka la pili ni kuomba na kupoke rushwa .
0 comments:
Post a Comment