BAADHI ya walimu wanaofundisha katika Shule za Sekondari za Katumba
na Nkeswa zilizopo katika kambi ya wakimbizi ya Katumba wilayani Mpanda
katika mkoa wa Katavi, wanatuhumiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na
wanafunzi wao wa kike.
Aidha imeelezwa kuwa mmoja wao “amemuoa” mwanafunzi wake kwa kumtolea
mahari kwa wazazi wake. Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) , George Kakunda alielezwa hayo na
Diwani wa Kata ya Katumba iliyopo katika Halmashauri ya Nsimbo, Seneta
Baraka wakati alipokutana na madiwani na watumishi wa halmashauri ya
Nsimbo katika majumuisho ya ziara yake ya siku moja aliyoifanya mkoani
Katavi.
Akimsimulia mikasa ya walimu hao, Diwani Baraka alisema: “Nilishatoa
taarifa ya mwalimu aliyemweka kinyumba mwanafunzi wake wa kike pia
walimu wenye mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wao wa kike katika
vikao vya baraza la madiwani, lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa
dhidi yao badala yake baadhi ya madiwani wenzangu wamevujisha siri za
vikao na kwenda kuwataarifu walimu hao kuwa mimi ndio ninayewashtaki,”
alieleza.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment