Tuesday, November 14, 2017

ALIYEKUWA AKIJIITA RIPOTA WA STAR TV NA MTOTO WA KAMANDA KOVA JELA MWAKA MMOJA KWA KUFANYA UTAPELI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na  Walter  Mguluchuma.
        Katavi .
  Aliyekuwa   akiita  Ripota wa  STAR  TV   wa  Mkoa  wa  Katavi  na  mtoto wa  Kamanda   Selemani  Kova   anaejulikana kwa  jina   la  Gerald  Kova  Mkazi wa  Mkoa wa  Mwanza  amehukumiwa  kifungo cha mwaka   mmoja  jela  baada ya kutiwa  hatiani  kwa kosa  la kufanya uapateli na kujipatia  mali kwa njia ya udanganyifu .
Hukumu  hiyo  ilitolewa hapo  jana  na  Hakimu   mfawidhi wa  Mahakama ya  Mwanzo   Mpanda   Marko  Pagyo  baada ya Mahakama  kulidhika  na  ushahidi uliotolewa  Mahakamani  hapo  na  upande wa  mashitaka .
Mwendesha  mashitaka wa  jeshi  la  Polisi    WP   Salima  alidai  Mahakamani  hapo  kuwa  mshitakiwa  huyo  alitenda  kosa hilo  hapo      Februari   8  mwaka  huu  katika   eneo la   Hotel ya   Madina   Manispaa ya  Mpanda.
  Ilidaiwa  kuwa   mshitakiwa  huyo  ambae   alikuwa   anajitambulisha  kuwa ni      mwakilishi wa   STAR   TV   yenye  Makao yake   makuu   Mkoani   Mwanza  na     ni   mtoto wa  Kamanda   Selemani  Kova alijipatia kwa  njia ya  udanganyifu   Kamera  moja   aina  ya   Canoni  yenye  thamani ya  Tshs  3,500,000   Lap   top  moja  na    stendi ya   Kamera ya   video  mali ya   Elias    Mlugala.
     Alisema   kuwa   mtuhumiwa   baada  ya  kuwa    amejipatia  mali  hizo kwa  njia ya   udanganyika   aliondoka  Mpanda   na kutokomea  kusiko   julikana huku   akiwa    ametapeli    kamera    nyingine     kwa   Eneresti  Kibada   aina  ya   Nikon   D   7,200   mali  ya  Chama  cha  Wandishi wa   Habari   Mkoa wa  Katavi yenye  thamani ya   Tshs  4,900.000.
Mwendesha  mashitaka  huyo   alieambia   Mahakama   mshitakiwa    baada  ya  kutokomea   haikujulikana   aliko  kuwa   amekimbilia   mpaka   hapo   mwezi      Agosti     alipokamatwa  huko  Kahama   na   huko   alikuwa   ajitambulisha kwa  jina  la  Crispin  Masawe na   alikamatwa baada ya  kuwa  amefanya  utapeli  mwingine wa kujipatia  kwa  njia ya  udanganyifu  Lap  top  moja ya  mwandishi wa   habari wa   Kahama .
  Alidai  kuwa    baada ya  kukamatwa    alfikishwa  katika    Mahakama ya   Mwanzo  ya  Hahama  na   kuhukumiwa  kifungo cha  miezi  mitatu    au  kulipa   faini ya    Tshs 100,000  hata  hivyo  hakuweza  kulipa na   alikwenda   gerezani .
  Mwendesha  mashita   alieleza  ndipo   Elias  na   Kibada   walipoa  taarifa  kituo cha  polisi cha   Mpanda juu  ya    mtuhumiwa  wao  kuhukumiwa   kifungo  hivyo walifanya  utaratibu na  waliweza  kwenda     Kahama na kumlipia  faini  hiyo na  kumtowa  gerezani na  kisha   akawa  chini ya ulinzi wa  polisi na   aliweza  kusarishwa  hadi   Mpanda  na  ndipo  alipofikishwa   Mpanda  na  Polisi   alipoweza   kuonyesha   vifaa      vyote   ambavyo   alikuwa   amemuuzia   mfanya  biashara  mmoja wa  huko  Maji  Moto   Wilayani  Mlele   Mkoani  hapa.
Mshitakiwa   Gerald  Kova  katika  utetezi wake   kabla ya kusomewa  hukumu   aliiomba  Mahakama   imwachie  huru kwa  kile    alichodai  kuwa      anakunywa    dawa ya  ARVs  kufubaza  maambukizi ya  ukimwi na   anamatatizo ya   ugonjwa wa      sikoseli    pia     mama  yake  mzazi ni  mgonywa   na   anamtegemea  yeye.
Baada  ya  utetezi huo   hakimu   Paragyo   alisoma  hukumu  na  kuamuru   mshitakiwa    atumikie  kifungo cha  mwaka  mmojs  jela  na   pindi   atakapo  toka   gerezani  atatakiwa  kulipa   Tshs   800,000.
  Mshitakiwa  huyo   anatarajiwa  kufikishwa    tena  mahakamani  hapo kwa   ajiri ya  kesi ya  pili  inayomkabili ya  kujipatia    kamera  Nicon  mali ya   Chama  cha  Wandishi wa  Habari    ambapo kesi  hiyo   itaendelea kusikilizwa.
MWISHO




No comments:

Post a Comment