WAVAMIZI 30 wamehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na Mahakama ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi baada ya kukiri makosa matano yaliyokuwa yakiwakabili ya kuishi kinyume cha Sheria ndani ya Hifadhi ya Luangwa River licha ya kutimuliwa mara kwa mara .
Makosa mengine waliyokuwa wakikabiliana nayo ni pamoja kujenga , kukata miti , kulima na kusihi bila ya kibali ndani ya hifadfhi hiyo .
Hakimu
wa mahakama hiyo , Teotimus Swai aliwahukumu washtakiwa hao kila mmoja
kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kukiri makosa yao .
Akihukumu alisema kuwa licha ya washtakiwa hao kutoisumbua mahakama kwa kukiri makosa yao lakini amelazimika kuwapatia adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama zao .
Awali Mendesha Mashtaka , Bakari Hongoli alidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao ikwa nyakati tofauti mwaka huu walitimuliwa kutoka hifadhini na kuamriwa na Mkuu wa Wilaya ya Mlele , Rachael Kasanga kutorejea tena hifadhini.
Ilielezwa mahakamani hapo kuwa lakini washtakiwa hao walikuwa wakikadi amri hiyo halali ya Mkuu wa Wilaya na kurejea hifadhini huku wakiendelea kufanya shughuli za kibinadamu ambaoz hazikuwa endelevu .
Mwisho
No comments:
Post a Comment