Walter Mguluchuma Na Arine Temu
Katavi .
Mampuni ya mafuta ya GBP imekabidhi kisima cha maji chenye thamani ya shilingi milioni 55 ikiwa ni msaada kwa ajiri ya Wakazi wa Kata ya Majengo Manispaa ya Mpanda chenye uwezo wa kutowa maji zaidi ya lita za ujazo 1,400 kwa siku .
Meneja wa Kampuni ya GBP alikabidhi kisima hicho hapo jana kwa niaba ya kampuni hiyo kwa Diwani wa Kata ya Majengo Willy Mbogo katika hafla iliyofanyika katika eneo la kisima hicho katika Mtaa wa Majengo
Katika hotuba yake wakati akikabidhi kisima hicho Meneja wa GBP Mpanda Hamad Nassor Said alisema kuwa kisima kicho kimegharimu kiasi cha shilingi milioni 55 na kinazalisha maji lita za ujazo 1460 kwa siku .
Alisema lengo la kampuni kutowa msaada huo kwa wananchi wa Kata hiyo ni katika kuwapunguzia wananchi tatizo la upungufu wa maji kwenye eneo la Kata hiyo ambayo ipo kati kati ya Mji wa Mpanda .
Meya wa Manispaa ya Mpanda Willy Mbogo ambae ni Diwani wa Kata ya Majengo aliishukuru kampuni hiyo kwa kutowa msaada huo muhimu wa kisima cha maji ambacho alisema kitakuwa ni msaada mkubwa si kwa wakazi wa Kata ya majengo peke yake bali na Kata zilizo jirani .
Alisema msaada huo ni muhimu kwani hakuna mtu yoyote duniani ambae kila siku hatumii maji kwa ajiri ya kunywa ,kuoga ,kufua na kupikia pamoja na kuoshea vyombo .
Mbogo aliwataka wananchi kuhakikisha wanatunza vizuri miundo mbinu hiyo kwani kumekuwa na tabia ya baadhi ya wananchi kutuma watoto kwenda kuchota maji na matokeo yake wamekuwa wakiharibu miundo mbinu hivyo wajenge tabia ya kuwatuma watoto wao wenye uwelewa na sio watoto wadogo zaidi .
Mwenyekiti wa Mtaa huo wa Majengo Maga Athanas alisema kuwa kisima hicho kitakuwa ni mkombozi kwa akina mama kwani walikuwa wakipata shida kubwa ya maji kutokana na eneo hilo la majengo kutokuwa na maji ya uhakika .
Nae Mashaka Rubuye alisema kuwa watu wengi watafaidika na maji ya kisima hicho kwani watu watakuwa wanachota bure tofauti na kwenye maeneo mengine ambapo maji huwa wanauziwa ndoo moja kati ya Tshs 200.
mwisho
0 comments:
Post a Comment